Ucsaf-Tanzania

Ucsaf-Tanzania

Share

UCSAF ilianzishwa na Serikali kwa lengo la kufanikisha huduma ya mawasiliano katika maeneo yasio na mvuto kwa watoa huduma ya mawasiliano nchini.

11/06/2026

๐Ÿ“Œ Tutakuwa mbashara kupitia Jogoo FM Redio- Ruvuma 93.0

11/06/2026

Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini. Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini, sasa imeanza utekelezaji wa Mradi wa Mawasiliano ya Simu Awamu ya Kumi, unaohusisha ujenzi wa minara 287 katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika utekelezaji wa mradi huo, mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imenufaika kwa kupata jumla ya minara 66 itakayojengwa ili kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo ambayo bado yana changamoto za mawasiliano.

Photos from Ucsaf-Tanzania's post 11/06/2026

KAMPENI YA ELIMU KWA UMMA MAENEO YA VIJIJINI.

Kampeni ya elimu kwa umma kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano na manufaa yake kwa wananchi, imeendelea katika baadhi ya vijiji vya mkoa wa Singida, Tabora na Kigoma, ambapo wananchi wamepewa elimu kuhusu manufaa ya huduma za mawasiliano zilizofikishwa katika maeneo yao na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote( UCSAF) kwa kushirikiana na watoa huduma.

Kampeni hiyo imefanyika kupitia mikutano ya vijiji, elimu ya mtu mmoja mmoja pamoja na katika maeneo yanayokusanya wananchi wengi kwa wakati mmoja k**a masoko, vituo vya usafiri na maeneo mengine ya shughuli za kijamii na kiuchumi.

Kupitia kampeni hiyo, wananchi wameelimishwa kuhusu matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano, fursa zinazotokana na intaneti na huduma za kifedha kwa njia ya simu, pamoja na mchango wa mawasiliano katika kuboresha maisha na kukuza shughuli za maendeleo katika jamii.

10/06/2026

๐Ÿ“Œ

09/06/2026

๐Ÿ“Œ Tufuatilie kupitia kipindi cha Redio Furaha Fm 96.7 MHz .

Photos from Ucsaf-Tanzania's post 09/06/2026

Wananchi wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wamefikiwa na kampeni ya elimu kwa umma inayolenga kuwaelimisha kuhusu manufaa ya huduma za mawasiliano kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini.

Kampeni hiyo imefanyika baada ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), kwa kushirikiana na watoa huduma za mawasiliano, kukamilisha mradi mkubwa wa ujenzi wa minara hiyo wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi.

Baadhi ya wananchi wa Kasulu wameleza kufurahishwa na maboresho ya huduma za mawasiliano katika maeneo yao, wakisema kuwa sasa wanaweza kuwasiliana kwa urahisi, kupata taarifa kwa wakati na kuendesha shughuli zao za kiuchumi kwa ufanisi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Serikali kupitia UCSAF imeendelea kusisitiza dhamira yake ya kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi wote bila kujali mahali walipo, hatua inayochangia kukuza uchumi wa kidijitali na kuimarisha ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo ya taifa.

Photos from Ucsaf-Tanzania's post 09/06/2026

Mhandisi Mwalami Kapipi kutoka Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini akizungumza na wasikilizaji wa Highlands FM (92.5) jijini Mbeya, ambapo amefafanua kwa kina utekelezaji wa miradi ya mawasiliano inayosimamiwa na UCSAF nchini. Katika mahojiano hayo, ameeleza pia maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambayo unajumuisha mkoa wa Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Songwe, Rukwa na Ruvuma.

Ameeleza kuwa miradi hiyo inalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo ya vijijini na yale ambayo hayana mvuto wa kibiashara kwa watoa huduma. Kupitia uwekezaji huo, wananchi wanawezeshwa kuwasiliana kwa urahisi zaidi, kupata taarifa muhimu kwa wakati, kutumia huduma za kifedha kwa njia ya kidijitali, pamoja na kunufaika na fursa za elimu, biashara na huduma nyingine za kijamii.

Aidha, miradi hiyo inaendelea kuchochea ukuaji wa uchumi wa maeneo husika na kuunga mkono jitihada za Serikali za kujenga Tanzania jumuishi ya kidijitali ambapo kila mwananchi anapata fursa sawa za kunufaika na maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano.

08/06/2026

๐Ÿ“ŒTufuatilie kupitia kipindi cha Redio.

05/06/2026

Serikali yaboresha Huduma za Mawasiliano katika Kijiji cha Shoga

Na Mwandishi Wetu,WMTH,Bungeni-Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaendelea kuboresha huduma za mawasiliano nchini katika maeneo mbalimbali, ikiwemo Kijiji cha Shoga, Jimbo la Rukwa. Kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Awamu ya Tisa ya Utekelezaji wa Miradi ya Mawasiliano Vijijini, ujenzi wa mnara wa mawasiliano unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2026.

Hayo yameelezwa leo, Juni 5, 2026, Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mk**a (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Rukwa Mhe. Masache Njelu Kasaka kwa niaba ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Aidha, Mhe. Dkt. Mk**a amesema kuwa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ulifanya ziara katika kijiji hicho na kujionea maendeleo ya mradi huo. Na kuongeza kuwa Mkandarasi anayetekeleza mradi ameahidi kukamilisha ujenzi wa mnara huo ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni 2026, hatua itakayosaidia kutatua changamoto ya mawasiliano iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa Kijiji cha Shoga na maeneo ya jirani.

Serikali imeeleza kuwa utekelezaji wa miradi ya mawasiliano vijijini ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za mawasiliano na kunufaika na fursa za Uchumi wa Kidijitali.
Reposted from

03/06/2026

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA MAWASILIANO KILOMBERO

Na Mwandishi Wetu-WMTH,Dodoma.

Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeendelea kuboresha huduma za mawasiliano katika Jimbo la Kilombero mkoani Morogoro kupitia utekelezaji wa Awamu ya Kwanza ya Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.

Hayo yameelezwa leo Juni 3, 2026, Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mk**a (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mhe. Abubakari Asenga Mbunge wa Jimbo la Kilombero kwa niaba ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Mhe. Dkt. Mk**a amesema kuwa kupitia mradi huo, mnara wa mawasiliano ulijengwa katika Kijiji cha Sagamaganga kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi wa eneo hilo na maeneo ya jirani.

Aidha, amesema kampuni ya Honora ilijenga mnara wa mawasiliano katika Kijiji cha Mherure ambao mnara huo unahudumia vijiji mbalimbali vinavyozunguka eneo hilo, hatua iliyochangia kuongeza wigo wa huduma za mawasiliano na kuimarisha mawasiliano kwa wananchi.

Ameongeza kuwa Aprili 8, 2026, UCSAF ilifanya tathmini katika Kijiji cha Mangula B na Kitongoji cha Ikwambi, ambapo ilibainika kuwa Kijiji cha Kanyenja kilijumuishwa katika Mradi wa Mawasiliano Vijijini wa minara 636. Mnara huo ulijengwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), huku baadhi ya maeneo katika vijiji hivyo yakitarajiwa kujumuishwa katika mipango ya kuimarisha huduma za mawasiliano ili kuongeza ubora na upatikanaji wa huduma hizo.

Vilevile Mhe. Dkt. Mk**a amesema Serikali itaendelea kufuatilia ubora wa huduma za mawasiliano katika maeneo husika ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na za uhakika.
Reposted from

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

Jengo La UCSAF, S. L. P 1957, 10 Barabara Ya UCSAF, Makulu
Dodoma
41107

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00