Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco

Share

Karibu kwenye ukurasa rasmi wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

12/06/2026

Zimebaki siku 4 tu kabla ya kuanza kwa mafunzo ya Kitaalam kwa Bodi na Watendaji wa Vyama vya ushirika kuhusu Uongozi, Kodi, Uhasibu na TEHAMA

Jisajili sasa

Mchoraji ✍️ CPA Philipo Alexander

Photos from Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco's post 12/06/2026

BODI YA WAKURUGENZI COASCO YASISITIZA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA UKAGUZI KWA VYAMA VYA USHIRIKA

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) imefanya kikao chake cha 86 kwa lengo la kupokea, kujadili na kuchambua taarifa mbalimbali ya kiutendaji ikiwemo ukaguzi, usimamizi wa vihatarishi, uchumi, mipango, ajira, maendeleo ya utumishi na utawala ili kuzidi kuimarisha utendaji wa Shirika.

Akiongoza kikao hicho Juni 11, 2026 kilichofanyika katika Ukumbi wa PSSSF, Dodoma, Mwenyekiti wa Bodi ya COASCO, CPA Juma A. Kimori, ambaye alishiriki kikao hicho kwa njia ya mtandao, amesisitiza Menejimenti kuendelea kutekeleza kwa wakati maelekezo na maamuzi ya Bodi ili kuboresha huduma za ukaguzi kwa vyama vya ushirika nchini.

CPA Kimori amesema kikao hicho kimejikita katika kupitia utekelezaji wa majukumu ya Shirika na kutathmini maendeleo yake, ambapo Bodi pia imeidhinisha masuala mbalimbali ya kiutendaji ikiwemo bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 pamoja na Mpango wa Manunuzi wa mwaka 2026/2027.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Jeremiah Mugeta, amesema Menejimenti itaendelea kutekeleza maelekezo yote ya Bodi na Serikali kwa wakati ili kuimarisha utendaji wa Shirika na kuongeza ubora wa huduma kwa wadau.

11/06/2026

Zimebaki siku 6 tu kabla ya kuanza kwa mafunzo ya Kitaalam kwa Bodi na Watendaji wa Vyama vya ushirika kuhusu Uongozi, Kodi, Uhasibu na TEHAMA

Jisajili sasa

Photos from Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco's post 09/06/2026

KAMATI YA BODI YA COASCO YAKUTANA KUJADILI MASUALA YA AJIRA, MAENDELEO YA UTUMISHI NA UTAWALA

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limeendesha kikao cha Kamati ya Bodi ya Ajira, Maendeleo ya Utumishi na Utawala kwa lengo la kupitia na kujadili masuala mbalimbali ya rasilimali watu, ajira, maendeleo ya watumishi, utawala pamoja na mpango wa mawasiliano na matumizi ya vyombo vya habari.

Kikao hicho kimefanyika leo, Juni 9, 2026 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Shirika jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa COASCO kinachotarajiwa kufanyika Juni 11, 2026.

08/06/2026

Zimebaki siku 8 tu kabla ya kuanza kwa mafunzo ya Kitaalam kwa Bodi na Watendaji wa Vyama vya ushirika kuhusu Uongozi, Kodi, Uhasibu na TEHAMA

Jisajili sasa

Photos from Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco's post 08/06/2026

KAMATI ZA BODI YA COASCO ZAPITIA NA KUJADILI TAARIFA ZA UKAGUZI, USIMAMIZI WA VIHATARISHI, UCHUMI NA MIPANGO

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limeendesha vikao vya Kamati ya Bodi ya Ukaguzi na Usimamizi wa Vihatarishi pamoja na Kamati ya Mipango na Uchumi kwa lengo la kupitia na kujadili ripoti ya Mkaguzi wa Ndani wa Shirika, taarifa ya usimamizi wa vihatarishi na taarifa ya utendaji wa Shirika.

Vikao hivyo vimefanyika leo, Juni 8, 2026 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Shirika jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa COASCO kinachotarajiwa kufanyika Juni 11, 2026.

07/06/2026

Zimebaki siku 9 tu kabla ya kuanza kwa mafunzo ya Kitaalam kwa Bodi na Watendaji wa Vyama vya ushirika kuhusu Uongozi, Kodi, Uhasibu na TEHAMA

Jisajili sasa

Photos from Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco's post 05/06/2026

*WATUMISHI WAPYA COASCO WAASWA KUZINGATIA WELEDI, UBUNIFU NA UADILIFU KAZINI*

*Watumishi wapya 10 wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) wameaswa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na uadilifu, kujenga uhusiano mzuri na wateja, kuzingatia mavazi ya utumishi wa umma na kutumia muda wa kazi ipasavyo ili kuongeza ufanisi wa Shirika.*

Rai hiyo imetolewa leo Juni 5, 2026 na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa COASCO, CPA Prisilla Mushi, wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya utumishi wa umma kwa watumishi wapya wa Shirika hilo.

CPA Prisilla amewahimiza watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa ubunifu na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea, huku wakizingatia uadilifu na uwajibikaji ili kuleta matokeo chanya katika utendaji wa Shirika.

“Muombe Mungu, fanya kazi kwa bidii, kuwa mbunifu na muaminifu katika utekelezaji wa majukumu yako, kuwa na uhusiano mzuri na wateja, na kuzingatia mavazi yanayoruhusiwa katika utumishi wa umma,” amesema CPA Prisilla.

Aidha, amewakumbusha umuhimu wa kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora ili kuimarisha afya zao, jambo litakalowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi.

Kwa upande wake, Ibrahim Mtale, kwa niaba ya watumishi wenzake, ameishukuru Menejimenti ya COASCO kwa kuandaa mafunzo hayo yaliyowaongezea uelewa kuhusu utumishi wa umma na shughuli za Shirika.

Mafunzo hayo yalianza Juni 4 na kuhitimishwa Juni 5, 2026, yakihusisha mada mbalimbali zilizowasilishwa na wakuu wa vitengo wa COASCO pamoja na wawakilishi kutoka PSSSF, TAKUKURU, TUICO, Maliwazo na ASF SACCOSS

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

2 Barabara Ya Hatibu,3 Madukani, S. L. P 761, Dodoma4110
Dodoma
4110