ushirika_tcdc

ushirika_tcdc

Share

T u me ya Ushirika

03/06/2026

Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD 2026) yanakaribia.

Hii ni nafasi ya kipekee kwa vyama vyote vya Ushirika kuonyesha mchango wao na kujifunza mbinu mpya za kiuchumi.

Malipo yafanyike kupitia benki ya CRDB
A/C NA. 0150429193900.
Jina la akaunti ni TFC - SUD TANZANIA

NB: Usisahau kuandika jina la chama.

Pamoja tujenge Uchumi.

Photos from Coop Bank Tanzania's post 03/06/2026
22/05/2026

Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Katika Jukwaa la Ushirika Dar es Salaam (2026)

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Ndg. Fares Muganda, akitoa salamu na mwelekeo wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania wakati akitoa hotuba yake wakati wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Dar es Salaam lililofanyika tarehe 20 Mei 2026.

Katika salam hizi, Ndg. Muganda anafafanua mikakati ya TFC katika kukuza uwakilishi na mashirikiano kuimarisha vyama vya ushirika, fursa za Biashara na Uwekezaji, na mchango wa kipekee wa vyama vya ushirika katika kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla katika kufikia Dira ya Taifa ya 2050.

20/05/2026

Mkopo Chap Chap ndani ya masaa 24 tu!

Mtumishi, pata mkopo hadi Tsh. 250 Milioni popote ulipo kwa kutumia mshahara wako. Omba kwa urahisi kupitia mfumo wa ESS (Employee Self Services) na timiza malengo yako sasa.

✅ Haraka
✅ Rahisi
✅ Salama

Je, ungefanya nini ukipata mkopo wako leo?

Mawasiliano Zaidi: +255 27 2754470

19/05/2026

Ofisini kwenu wanajua hili?
Sasa unaweza kulipa mishahara ya wafanyakazi hadi 1000 kwa mkupuo mmoja kwa urahisi, usalama na haraka kupitia huduma ya Benki Mtandao (Internet Banking)

Punguza usumbufu wa malipo na ongeza ufanisi wa biashara yako leo!

Wasiliana nasi upate huduma bora za kibenki kwa biashara yako. +255 27 27 54470

Photos from ushirika_tcdc's post 17/05/2026

TCDC YAIBUKA MSHINDI WA PILI 'MWENGE CUP' DODOMA

Timu ya soka ya TCDC Sports club imeibuka mshindi wa pili kwenye mashindano ya Mwenge CUP yaliyofanyika Jijini Dodoma.

Timu Mpira wa Miguu ya TCDC imecheza Leo Mei 17, 2016 mchezo wa fainali dhidi ya Wizara ya Ujenzi kufungwa goli moja na kuwa mshindi wa pili katika Mashindano ya Mwenge Cup Dodoma.

Photos from ushirika_tcdc's post 16/05/2026

NENDENI KIFUA MBELE MKAUTANGAZE USHIRIKA KUPITIA STAKABADHI ZA GHALA - CHIPOLA

Viongozi wa Chama na Serikali wa mkoa wa Dodoma wamehimizwa kuendelea kuutangaza Ushirika kupitia wananchi hususan wanaowahudumia kwa kujiunga na Vyama vya Ushirika na kuuza mazao yao kupitia Mfumo wa stakabadhi za ghala na hivyo kujikwamua kiuchumi na kuleta Maendeleo ya mtu mmojammoja na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa Mei 14, 2026 na Mwenyekiti wa Bodi wa Chama Kikuu cha Ushirika (TANECU LTD) Karimu Chipola alipokuwa akifungua kikao kilichohusisha Mafunzo ya Mfumo wa Stakabadhi za kwa Viongozi hao yaliyofanyika katika ghala la Chama hicho wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.

Amesema kwasasa Ushirika umeimarika kwakuwa Viongozi wanazingatia weledi na uadilifu na hivyo kupunguza malalamiko ya wanaushirika na wakulima,ombi langu sasa kupitia Mafunzo haya nendeni mkautangaze ushirika katika maeneo yenu na Manufaa yake na Mfumo wa stakabadhi za ghala ili wakulima waweze kunufaika.

Kwa upande wake Mwendesha Ghala ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Bin Swalehe General Dealers LTD Simon Nkana ameeleza Utaratibu na Muundo wa Utekelezaji Mfumo ikiwemo Usajili wa awali, Uhakiki na Udaralidhaji, Upimaji kupitia mizani, kushusha mzigo stoo na taarifa za utoaji risiti.

Awali Viongozi hao walipata fursa ya kutembelea Bodi ya Korosho Tanzania ( CBT) , na mradi wa ujenzi wa maghala mawili ya kuhifadhia Korosho ya TANECU yanayojengwa katika vijiji Mchichira, Mnyawa na Mkonjowano wilayani Tandahimba mkoani humo.

Photos from ushirika_tcdc's post 16/05/2026

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga, ametoa amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kusimamia taasisi hizo kwa weledi na uaminifu na kusisitiza umuhimu wa viongozi kupata elimu ya mara kwa mara ili kuongeza ufanisi.

Maagizo yametolewa kwa Niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Michael Semindu, 15 Mei, 2026 alipokuwa akihitimisha jukwaa la vyama vya Ushirika mkoani humo kwa mwaka 2026.

Aidha, Viongozi wa Vyama wametakiwa kuepuka vitendo vya upendeleo wakati wa kutekeleza majukumu yao na kuwa ushirika imara unategemea uongozi unaofuata misingi ya haki na uwazi ili kujenga imani kwa wanachama.

​Aidha, Mhe. Semindu amewakumbusha maafisa ushirika kutoegemea upande wowote na kuepuka kuwa chanzo au sehemu ya migogoro inayovikabili vyama hivyo, badala yake wawe wasuluhishi na washauri wa kitaalamu.

​Kwa upande mwingine, wadau wa ushirika wameiomba Serikali kuingilia kati na kuweka mikakati thabiti ya kuhamasisha vijana kujiunga na sekta hiyo ili kuhakikisha inarithishwa kwa kizazi kijacho. Wanaushirika hao wamebainisha kuwa ushiriki wa vijana ni nguzo muhimu katika kuleta ubunifu na nguvu mpya itakayosaidia kuendeleza ushirika nchini.

Photos from ushirika_tcdc's post 15/05/2026

WANAUSHIRIKA KILIMANJARO WAPATIWA ELIMU YA USHIRIKA KUHUSU USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA VYAMA

Wanaushirika wakiwemo Wanachama wa SACCOS na AMCOS Mkoani Kilimanjaro wamepatiwa Elimu kuhusu masuala mbalimbali yanahohusu Ushirika.

Hayo yamefanyika leo Mei 15, 2026 katika siku ya pili ya kuhitimisha Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani humo.

Wawezeshaji waliotoa Elimu ni pamoja na Mkuregenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Miriam Mmbaga ameelezea kuhusu Mwongozo wa Ajira na utendaji, haki, wajibu na majukumu ya mwajiri na mwajiriwa.

Liliani Lyimo, Afisa Sheria kutoka TCDC ametoa Elimu kuhusu mabadiliko ya Sheria ya vyama vya Ushirika na toleo Rekebu la Mwaka 2025, haki na majukumu ya mwanachama na mamlaka ya Mrajis wa vyama vya Ushirika.

Naye Daudi Ramadhani, Afisa Tehama kutoka TCDC ameelezea kuhusu Mfumo wa Vyama vya Ushirika (MUVU). Namna ya kujiunga, vipengele vinavyofanyiwa marekebisho na namna unavyofanya kazi.

Pia walikuwepo wawezeshaji wengine ambao kutoka Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Bima ya Afya (NHIF), Chama Kikuu cha Ushirika cha Akiba na mikopo Tanzani (SCCULT), Shirikisho la vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Waadhiri kutoka chuo cha Ushirika moshi (MoCU), Kampuni ya Bima (BUMACO), na Benki ya Ushirika Tanzania (COOP BANK).

Photos from ushirika_tcdc's post 15/05/2026

Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) inaendelea kutoa elimu ya kuwajengea uwezo wanaushirika visiwani Zanzibar kupitia mafunzo maalum ya kisekta.

Mafunzo haya yana lengo la kuimarisha utendaji na tija ndani ya vyama vya ushirika

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address

Kuu Street
Dodoma