13/06/2026
e-GA inakusudia kutekeleza afua mbalimbali ili kusaidia taasisi za umma kutoa huduma mtandao kwa ufanisi. ISO 9001: 2015
CERTIFIED
13/06/2026
05/06/2026
Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), leo tarehe 5 Juni 2026, wamepatiwa elimu kuhusu ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) na wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Ikulu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, jijini Dodoma.
Elimu hiyo imelenga kuongeza uelewa kuhusu njia za maambukizi, dalili, kinga na umuhimu wa kupata huduma za uchunguzi na matibabu mapema. Aidha, watumishi waliopo nje ya Dodoma walishiriki mafunzo hayo kwa njia ya mkutano wa video (video conference) na kupitia mfumo wa e-Mikutano.
cc,
30/05/2026
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Dkt. M***a Kissaka (kulia), akikabidhiwa rasmi Ripoti ya Ukaguzi wa Taarifa ya Fedha ya Mamlaka ya Mwaka wa Fedha 2024/2025, ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) yenye Hati Safi, na Mkurugenzi Mkuu wa e-GA Mhandisi Benedict Ndomba, ikiwa ni uthibitisho wa uwajibikaji, uwazi na usimamizi bora wa rasilimali za taasisi.
Makabidhiano hayo yamefanyika Mei 29, 2026 jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bodi hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray, ameliambia Bunge kwamba Serikali inaendelea kuboresha matumizi ya Serikali Mtandao, ili kurahisha upatikanaji wa huduma za Serikali kwa wananchi wa vijijini.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Dk. Catherine Joachim, Mhe.Qwaray amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imetekeleza jitihada mbalimbali za ujenzi wa Serikali Mtandao ikiwemo, kubuni mifumo ya TEHAMA inayoweza kutumiwa na Wananchi katika mazingira yote ya mijini na vijijini.
19/05/2026
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Ndege Qwaray (Mb), amefanya ziara ya kikazi katika Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji wa Serikali Mtandao (Research, Innovation and Development Centre – RIDC) kilichopo jijini Dodoma, ambapo amekagua miradi mbalimbali ya TEHAMA inayotekelezwa na kituo hicho kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma Serikalini.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Mei 18, mwaka huu, Mhe. Qwaray alipata fursa ya kutembelea na kujionea miradi ya kiteknolojia inayolenga kutoa suluhisho kwa changamoto katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya na utawala.
Aidha, miradi hiyo inahusisha matumizi ya teknolojia zinazochipukia k**a vile Internet of Things (IoT) na Akili Mnemba (AI), katika kurahisisha utendaji kazi Serikalini na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Qwaray ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa juhudi zake za kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana, kupitia tafiti na ubunifu wa mifumo mbalimbali ya TEHAMA yenye mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.
07/05/2026
Leo (Mei 07,2026) siku ya Tatu ya Mkutano Mkuu wa Pili Jumuishi wa Mwaka wa Jumuiya za Wataalamu wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, katika Utumishi wa Umma Tanzania, wananchi mbalimbali wametembelea banda la e-GA na kupatiwa msaada wa kiufundi pamoja na Elimu ya Matumizi ya TEHAMA
#
| Monday | 07:30 - 15:30 |
| Tuesday | 07:30 - 15:30 |
| Wednesday | 07:30 - 15:30 |
| Thursday | 07:30 - 15:30 |
| Friday | 07:30 - 15:30 |