"Utafiti ndiyo Moyo wa Sekta ya Madini, kwa mara ya kwanza. Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeipa Sekta ya Madini fursa ya kubakiza asilimia 10 ya maduhuli inayokusanya kwa ajili ya kuendesha shughuli za utafiti, hatua inayochochea ukuaji na ushindani wa sekta hiyo." Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde.
&Utajiri
Wizara ya Madini
Sekta ya Madini kwa Uchumi Imara na Maendeleo Endelevu
"Ili Sekta ya Madini iweze kufanikiwa zaidi lazima iwekeze kwenye watu wa chini ambao ni wachimbaji wadogo."
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.
Wadogo
MadininiMaisha&Utajiri
14/06/2026
STAMIGOLD YAANDIKA HISTORIA YAONGEZA UHAI WA MGODI HADI 2032
● Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yaipongeza kwa uwekezaji wa mitambo ya kisasa
● *Yatajwa kurefusha uhai wa mgodi kwa miaka sita zaidi kupitia ugunduzi wa mashapo mapya*
● *Yatoa ajira 740 kwa wazawa, yagundua akiba mpya ya wakia 100,319*
*Bihalamuro*
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Kampuni ya Uzalishaji Dhahabu ya STAMIGOLD inayosimamiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kufuatia mafanikio makubwa ya uzalishaji wa dhahabu na kurefusha uhai wa mgodi hadi mwaka 2032.
Pongezi hizo zilitolewa Juni 13, 2026 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Subira Mgalu, wakati wa ziara maalum ya wajumbe wa kamati hiyo iliyolenga kukagua shughuli za uzalishaji madini katika mgodi huo uliopo wilayani Biharamulo.
Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Mgalu aliitaka STAMICO kuendelea kufanya utafiti wa kina katika maeneo ya leseni zake zilizotengwa ili kupata taarifa mpya zitakazowezesha kuanzisha mgodi mwingine mpya wa dhahabu ili kuendelea kuimarisha kampuni ya STAMIGOLD.
Pia, alishauri STAMICO kuendeleza uwekezaji katika sekta ya madini kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo hususan kwenye utafiti wa madini mkakati ili kuongeza idadi ya migodi itakayosaidia katika maendeleo ya uchumi kwa taifa.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, aliishukuru Kamati ya Bunge kwa ushauri wake wa kiufundi na kubainisha kuwa Wizara ya Madini itaendelea kupokea maoni na ushauri huo ili kuendeleza sekta, hususan kwenye maeneo ya ushirikiano wa kimkakati katika uwekezaji kupitia taasisi zake za utendaji.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO, Dkt. Venance Mwase, alieleza kuwa mgodi unaendelea na uhakiki pamoja na utafiti ndani ya leseni maalum ya uchimbaji kwa kutumia njia mbalimbali za ukusanyaji wa taarifa na ukadiriaji upya ili kuongeza taarifa za akiba ya mashapo ya mgodi huo.
Awali, akiwasilisha taarifa ya utendaji ya kampuni hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa STAMIGOLD Ali Ali alisema kuwa kuanzia mwezi Julai 2014 hadi Mei 2026, jumla ya wakia 137,049.73 za dhahabu zimezalishwa.
Ali aliongeza kuwa, mgodi umefanikiwa kuongeza ufanisi kwa kununua mtambo mkubwa wa kisasa.
14/06/2026
STAMIGOLD YAANDIKA HISTORIA YAONGEZA UHAI WA MGODI HADI 2032
● Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yaipongeza kwa uwekezaji wa mitambo ya kisasa
● Yatajwa kurefusha uhai wa mgodi kwa miaka sita zaidi kupitia ugunduzi wa mashapo mapya
● Yatoa ajira 740 kwa wazawa, yagundua akiba mpya ya wakia 100,319
📍Biharamulo
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Kampuni ya Uzalishaji Dhahabu ya STAMIGOLD inayosimamiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kufuatia mafanikio makubwa ya uzalishaji wa dhahabu na kurefusha uhai wa mgodi hadi mwaka 2032.
Pongezi hizo zilitolewa Juni 13, 2026 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Subira Mgalu, wakati wa ziara maalum ya wajumbe wa kamati hiyo iliyolenga kukagua shughuli za uzalishaji madini katika mgodi huo uliopo wilayani Biharamulo.
Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Mgalu aliitaka STAMICO kuendelea kufanya utafiti wa kina katika maeneo ya leseni zake zilizotengwa ili kupata taarifa mpya zitakazowezesha kuanzisha mgodi mwingine mpya wa dhahabu ili kuendelea kuimarisha kampuni ya STAMIGOLD.
Pia, alishauri STAMICO kuendeleza uwekezaji katika sekta ya madini kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo hususan kwenye utafiti wa madini mkakati ili kuongeza idadi ya migodi itakayosaidia katika maendeleo ya uchumi kwa taifa.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, aliishukuru Kamati ya Bunge kwa ushauri wake wa kiufundi na kubainisha kuwa Wizara ya Madini itaendelea kupokea maoni na ushauri huo ili kuendeleza sekta, hususan kwenye maeneo ya ushirikiano wa kimkakati katika uwekezaji kupitia taasisi zake za utendaji.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO, Dkt. Venance Mwase, alieleza kuwa mgodi unaendelea na uhakiki pamoja na utafiti ndani ya leseni maalum ya uchimbaji kwa kutumia njia mbalimbali za ukusanyaji wa taarifa na ukadiriaji upya ili kuongeza taarifa za akiba ya mashapo ya mgodi huo.
Awali, akiwasilisha taarifa ya utendaji ya kampuni hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa STAMIGOLD Ali Ali alisema kuwa kuanzia mwezi Julai 2014 hadi Mei 2026, jumla ya wakia 137,049.73 za dhahabu zimezalishwa.
inaendelea kwenye comments...
"Tunajipanga kuihamishia Dubai Tanzania," .Msikilize Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde akifafanua ni kwa namna gani.
&Utajiri
WachimbajiWadogo
13/06/2026
"Mpango unaozinduliwa leo ni wa kihistoria kwani unaweka dira ya maendeleo ya wachimbaji wadogo wa madini kwa kipindi cha miaka 25 ijayo. Tunapongeza juhudi za Wizara ya Madini chini ya uongozi wa Waziri mwenye dhamana kwa kuendelea kuweka mazingira bora ya ukuaji wa sekta hii muhimu. Mkoa wetu umeendelea kunufaika na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotokana na sekta ya madini, sambamba na ongezeko la mapato yanayokusanywa kupitia shughuli za madini, jambo linalochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi," Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo.
&Utajiri
13/06/2026
"Leo ni siku ya kipekee kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini. Timu ya wataalamu iliyoundwa mahsus kwa ajili ya kuandaa mapendekezo ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo imekamilisha kazi yake na tunatarajia kupokea ripoti ambayo ni matokeo ya kazi kubwa iliyofanywa kwa weledi na utaalamu wa hali ya juu. Nina imani kuwa mapendekezo yaliyomo katika ripoti hii yatakuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha sekta ya uchimbaji mdogo wa madini na kuongeza tija kwa wachimbaji wetu, kwa kuzingatia uzoefu na umahiri wa wataalamu waliounda timu hiyo."Katibu Mkuu, Wizara ya Madini ,Eng. Yahya Samamba.
&Utajiri
Yanayojiri sasa katika Hafla ya Kupokea Ripoti ya Mapendekezo ya Kuwaendeleza Wachimbaji wadogo wa Madini Nchini.
13/06/2026
📍 Dar Es Salaam.
Baadhi ya Wageni na Viongozi mbalimbali tayari wamewasili katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki katika hafla ya kupokea Ripoti ya Mapendekezo ya Kuwaendeleza Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini.
Growth
13/06/2026
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Website
Address
255