13/05/2026
Wakaazi wa kijiji cha Mikinduni eneo la Majembeni katika kaunti ya Lamu wanalalamikia changamoto ya mimea yao kushambuliwa na kuliwa na Ndovu walikithiri eneo hilo.
Wameeleza kwamba ni takriban muda wa mwaka mmoja sasa mahangaisho ya Ndovu yameendelea kushudiwa eneo hilo huku wakipoteza mavuno yao.
13/05/2026
Polisi kutoka kituo cha polisi cha Mtwapa kaunti ya Kilifi wamewakamata washukiwa watatu wa ulanguzi wa dawa za kulevya na kufanikiwa kupata bangi iliyokuwa imefungwa na kufichwa kwa ajili ya biashara.
Washukiwa hao ni Abdi Hadji Boru mwenye umri wa miaka 37, Ephantus Kamau maarufu Raila mwenye miaka 22 pamoja na David Juma Odhiambo mwenye miaka 29
13/05/2026
Kijana mmoja mhudumu wa bodaboda amepoteza maisha papo hapo baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani eneo la Changamwe Roundabout mapema leo.
Kulingana na mashuhuda, kijana huyo alikuwa akitokea katikati mwa jiji la Mombasa ambapo aligongwa na lori na kufariki papo hapo
13/05/2026
Tuko Bomba ndo habari ya mjini ...mda wa kutetemesha anga kwa mirindimo ya kimwambao tayari nipo nyuma ya bomba ndio maana tunasema Tuko Bomba niite Malkia Emma Marevu. Upo hapo ulipo?
13/05/2026
Man City leo wataamua tupee wale jamaa kombe ama waendelee kusubiri kiasi. Mida ni ya Kutubuti na Captain Lolo
13/05/2026
Imeibuka kuwa wanafunzi wa shule 12 za eneo la pwani walipanga kupitia Whatsapp group jinsi watachoma mabweni ya shule. Wanafunzi 33 wameshtakiwa kotini, na wazazi watagharamikia hasara iliyotokana na moto katika shule hizo. Hawa Wanafunzi watarekebishwa vipi??