Swahili MEDIA

Swahili MEDIA

Share

πŸ”΄ HABARI, MATUKIO NA MICHEZO
🟒 MAWASILIANO PIGA:0713114698
πŸ”΅

15/06/2026

Kijana mmoja aitwaye Lameck Jonathan Mlay (30) mfanya usafi wa bar na mkazi wa Maji ya Chai mkoani Arusha anadaiwa kumuua Husna Shabani (33) mkazi wa Majengo Jijini Arusha na kisha kutupa mwili huo katika chemba ya maji taka iliyopo katika bar hiyo.

SWAHILI MEDIA imefika eneo la tukio na kuzungumza na wajumbe wa serikali wa mtaa wa samanga ilipo bar hiyo na kudai kuwa walifika na kuonyeshwa video za cctv camera ikimuonyesha mtuhumiwa huyo akifanya tukio Hilo.

Aidha Akitoa taarifa hiyo leo Juni 15, 2026 Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 14, 2026 muda wa jioni huko katika Bar iitwayo Sh**ha Village iliyopo kata Elerai Jijini Arusha.

Kaamanda masejo Ameendelea kufafanua kuwa uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo umebaini kuwa kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa na marehemu walikuwa pamoja kwenye starehe katika eneo hilo, huku akibainisha wanakamilisha uchunguzi kwa taratibu nyingine za kisheria.

15/06/2026

🚨_π—’π—™π—™π—œπ—–π—œπ—”π—Ÿ & π—–π—’π—‘π—™π—œπ—₯π— π—˜π—— βœ…πŸ‘‡

Mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga SC vs Azam FC rasmi umethibitishwa kuchezwa visiwani Zanzibar Dimba la New Amani Complex

Awali Yanga SC waliomba uchezwe CCM Kirumba ila ombi likagonga mwamba

Yanga SC na Azam FC wakitoka Mwanza wataelekea Zanzibar

14/06/2026

Mtazamaji wa SWAHILI MEDIA leo JUNE 14 2026 tumefika tena katika kanisa la Mchungaji Salome Kikoto, ambaye ameendelea kugusa mioyo ya watu wengi kufuatia kitendo chake cha kishujaa cha kumuokoa kijana Kelvin aliyekuwa katika hatari ya kuuawa na wananchi baada ya kutuhumiwa kwa wizi. Tukio hilo lililovuta hisia za Watanzania wengi limeifanya huduma ya mchungaji huyo kuendelea kupata uungwaji mkono kutoka kwa watu mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Arusha.

Katika ziara hiyo, wageni mbalimbali walifika kanisani hapo wakiongozwa na mwanadada Resty Bura kutoka Dar es Salaam, ambaye alikabidhi rasmi michango mbalimbali iliyotolewa na Watanzania wenye mapenzi mema kwa ajili ya kuunga mkono huduma hiyo. Mbali na michango ya wadau wengine, Resty naye alichangia kwa moyo wa kujitolea, akisisitiza umuhimu wa kuthamini na kusapoti watu wanaojitoa kusaidia jamii katika nyakati ngumu.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Resty Bura aliwaomba Watanzania kuendelea kushik**ana na kuisapoti huduma ya Mchungaji Salome Kikoto, akieleza kuwa kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kurudisha fadhila na kuthamini wema aliouonyesha kwa kuokoa maisha ya kijana Kelvin . Alisema matendo ya huruma na utu k**a hayo yanapaswa kuungwa mkono ili yawe chachu ya kuhamasisha upendo, mshik**ano na kusaidiana katika jamii.

14/06/2026

WAUMINI WA KANISA LA KILUTHERI AFRIKA MASHARIKI MOSHONO JIJINI ARUSHA WAMEPATA NA TAHARUKI BAADA YA KUKUTA WATU WANAODAIWA KUWA DALALI WA MAHAKAMA WAKIWA WAMETOA VITU VYOTE VILIVYOMO NDANI YA KANISA HILO HUKU WAKIENDELEA NA UJENZI WA UZIO KUZUNGUKA ENEO HILO KWA MADAI KUWA MTU ALIYETOA ENEO HILO SIYO MALI YAKE KITENDO KILICHO ZUA MALUMBANO MAKALI KURUSHIA MANENO KUSHIKANA NA KUANGUSHANA CHINI KATI YA DALALI MKANDARASI WA UJENZI HUO NA FAMILIA INAYODAIWA KUMILIKI KIWANJA HICHO AMBAO NI SEHEMU YA VIONGOZI WA KANISA HILO

13/06/2026

Halmashauri ya Jiji la Arusha imetakiwa kuharakisha upatikanaji wa fedha kwa mkandarasi aliyepewa zabuni ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Osunyai ili kukamilisha mradi huo na kuondoa msongamano mkubwa wa wanafunzi unaoendelea kuathiri mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji shuleni hapo.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Osunyai, Elirehema Nnko, alisema mradi huo ulitengewa zaidi ya Sh milioni 360 katika mwaka wa fedha 2024/2025 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ghorofa la madarasa.

Aidha walimu wa Taaluma wa shule hiyo, Rebeka Shoo amesema kuwa zaidi ya madarasa nane yalivunjwa kupisha mradi huo, huku shule ikiwa na zaidi ya wanafunzi 3,000, jambo ambalo limeongeza msongamano mkubwa katika vyumba vilivyobaki.

12/06/2026

πŸš¨πŸ’£π”ππƒπ€π“π„: Yanga wako kwenye hatua nzuri sana za kukamilisha usajili wa Aziz Ki kutoka Libya.

Ndani ya hizi siku chacha Aziz Ki atatua nchini…..possibly weekend hii anaweza kuingia Tanzania.

Yanga na Aziz Ki kuna kitu hivi karibuni
Ameandika hans rafel

12/06/2026

Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, amesema ushindani wa Ligi Kuu ya NBC umekuwa mkubwa zaidi, akieleza kuwa Simba SC imeonyesha maendeleo makubwa katika mbinu, nidhamu ya mchezo na mfumo wa benchi la ufundi ikilinganishwa na misimu iliyopita.

Kutokana na kuridhishwa na kazi yake na dira ya muda mrefu ya klabu, Azam FC imempa Ibenge mkataba mpya utakaomuweka Chamazi hadi mwaka 2028, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwania kuvunja ubabe wa timu za Kariakoo katika soka la Tanzania.

12/06/2026

πŸš¨π™π™π˜Όπ™‰π™Žπ™π™€π™ π™‰π™€π™’π™Ž: Klabu ya Simba SC imeanza kufanya mazungumzo ya awali na kiungo mshambuliaji mkongwe wa Afrika Kusini, Themba Zwane maarufu kwa jina la β€œMshishi”, kuhusu uwezekano wa kuhamia Msimbazi kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 36, ambaye amejijengea heshima kubwa ndani ya soka la Afrika akiwa nahodha na mmoja wa wachezaji muhimu wa klabu ya Mamelodi Sundowns, yuko katika hatua za kutathmini hatma yake ya baadaye baada ya kuitumikia timu hiyo kwa zaidi ya muongo mmoja.

Zwane, anayejulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao, pasi za mwisho zenye ubora wa hali ya juu na uongozi ndani ya uwanja, amekuwa miongoni mwa viungo bora kuwahi kutokea Afrika Kusini. Katika kipindi chake akiwa Mamelodi Sundowns, ameshinda mataji mengi ya ligi ya Afrika Kusini pamoja na ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, huku pia akiitumikia timu ya taifa ya Afrika Kusini kwa zaidi ya mechi 50.

Chanzo cha karibu na mchezaji huyo kinaeleza kuwa Simba inavutiwa na uzoefu wake mkubwa wa kimataifa pamoja na uwezo wake wa kuiongoza safu ya kiungo katika mashindano makubwa ya Afrika. Uongozi wa Wekundu wa Msimbazi unaaminika kuona kuwa ujio wa Zwane unaweza kuongeza ubora, utulivu na uzoefu ndani ya kikosi kinachojiandaa kwa ushindani mkubwa wa ndani na kimataifa.

Licha ya umri wake kufikia miaka 36, β€œMshishi” bado anaendelea kuaminiwa katika kikosi cha Mamelodi Sundowns na hata timu ya taifa ya Afrika Kusini, jambo linaloonyesha kiwango chake bado kinaheshimika ndani ya soka la bara hili. Hivi karibuni alijumuishwa katika kikosi cha Afrika Kusini kuelekea mashindano ya Kombe la Dunia 2026 kutokana na uzoefu wake mkubwa.

Iwapo mazungumzo hayo yatazaa matunda, Zwane atakuwa mmoja wa wachezaji wenye wasifu mkubwa zaidi kuwahi kujiunga na Simba katika miaka ya karibuni. Mashabiki wa Simba tayari wameanza kufuatilia kwa karibu taarifa za kiungo huyo, wakiamini kuwa anaweza kuwa nyongeza muhimu katika safari ya klabu hiyo ya kutafuta mafanikio makubwa zaidi ndani ya Afrika.

12/06/2026

FIFA imeitaka Timu ya FC Lupopo iwalipe Yanga SC Kiasi cha Dollars 55,000 sawa na milioni 144 za kitanzania baada ya kudanganya umiliki wa Beki Chadrack Boka ambae alikuwa anamilikiwa na AS REAL KINSHASA, Wakati Klabu ya Yanga inamsajili Chadrack Boka FC Lupopo iliwaambia Boka ni mchezaji wao kwa asilimia 100% hivyo Yanga SC wakailipa FC Lupopo angali haikuwa inammiliki mchezaji huyo.

Baadae Yanga SC iliwalipa AS Real Kinshasa waliokuwa wamiliki Halali wa Chadrack Boka ndipo Yanga SC iliposh*taki FIFA na FIFA kuitaka FC Lupopo ilirudishe Dollar 50,000 za Yanga SC na faini ya Dollars 5000.
FC Lupopo inatakiwa ilipe Dollar 50,000 ambazo Yanga walizilipa na faini ya Dollars 5000.

Yanga SC imeshinda Kesi na FC Lupopo ambapo FIFA imesema fedha hizo zinapaswa kulipwa ndani ya siku 45.

✍️Nassib mkomwa

12/06/2026

hali ya sintofahamu imetokea katika mtaa wa RC Kata ya Olorieni jijini Arusha baada ya mzee mmoja aliyefahamika kwa jina la Felix Moses Ngoo, ambaye inaelezwa kwamba alijifanya balozi katika eneo hilo,na kujichukulia pesa katika nyumba ambayo ilikuwa na mgogoro kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili. Kwa mujibu wa mashuhuda pamoja na watu ambao wamedai kwamba wametapeliwa na mzee huyo. imeelezwa kwamba kwa kipindi cha muda mrefu

Felix Ngoo, ambaye inaelezwa kwamba alikuwa akitumia nafasi ya ubalozi vibaya, amesema kwamba yeye alichaguliwa na chama cha Mapinduzi na hawatambui wale waliokuwa wakimfukuza.

Want your business to be the top-listed Government Service in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Arusha