14/05/2026
β³ BADO SIKU 03 PEKEE! β³
Muda unazidi kusonga kuelekea tukio kubwa la Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya WRRB! π
π Tukutane JKCC, Dodoma kuanzia Mei 17 - 19, 2026. Njoo tujadili na kujifunza zaidi kupitia kaulimbiu yetu inayoongoza maadhimisho haya: βMfumo Imara, Uchumi Endelevuβ. Usipange kukosa!
14/05/2026
TAARIFA KWA UMMA
.hmwinyi
13/05/2026
Muda unayoyoma kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB)! π
Ni miongo miwili ya kuleta mapinduzi na uhakika katika sekta ya kilimo na biashara nchini Tanzania πΉπΏ. Tunaenda kuadhimisha hatua hii kubwa tukiangazia ukuaji na tija kwa wakulima na wafanyabiashara wetu.
ποΈ Tarehe: 17 β 19 Mei, 2026
π Mahali: Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), Dodoma
π‘ Kaulimbiu: βMfumo Imara, Uchumi Endelevu.β
Wadau wote wa kilimo, biashara, na uchumi mnaombwa mkae mkao wa kula!
Je, wewe utakuwepo Dodoma kuungana nasi?
Dondosha comment yako hapa chini au tag mdau ambaye hapaswi kukosa hii! ππΎ
12/05/2026
Zimebaki siku 5 pekee kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB)! π
Kwa miongo miwili, tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wakulima na wafanyabiashara wanapata tija kupitia mfumo rasmi na salama. Ungana nasi katika kuadhimisha hatua hii muhimu huku tukijadili mustakabali wa sekta ya kilimo na biashara nchini Tanzania.
ποΈ Tarehe: 17 β 19 Mei, 2026
π Mahali: Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), Dodoma
π‘ Kaulimbiu: Mfumo Imara, Uchumi Endelevu.
WizaraYaViwandaNaBiashara
11/05/2026
ποΈ Bado siku 06 kuelekea Miaka 20 ya kujenga mifumo imara kwa maendeleo endelevu. β¨
Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) inaadhimisha miaka 20 ya mafanikio, ubunifu na mchango katika kukuza biashara, kilimo na uchumi wa Tanzania. πΉπΏ
π Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), Dodoma
π
17β19 Mei 2026
ποΈ Bado siku 06
09/05/2026
Leo Mei 9 2026, Bw. Asangye Bangu,Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala(WRRB) pamoja na watumishi wa Bodi hiyo wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa ajili ya kufanya utalii wa ndani na kupata muda wa kupumzika baada ya kipindi kirefu cha utekelezaji wa majukumu ya kazi.
Ziara hiyo imelenga kuwajengea watumishi ari mpya ya kazi, kuimarisha ushirikiano pamoja na kuwapa fursa ya kufurahia vivutio vya utalii vilivyopo nchini. Aidha, watumishi walipata nafasi ya kujionea wanyamapori mbalimbali na mandhari ya kuvutia yaliyopo katika hifadhi hiyo.
.hmwinyi
08/05/2026
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Aristides Mbwasi amefungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Mei 8, 2026, kilichofanyika katika Ukumbi wa Edema mkoani Morogoro.
Aidha katika Kikao hicho cha Baraza pia kimejadili Bajeti ya mwaka 2026/2027 pamoja na kujadili namna bora ya kutatua kero mbalimbali za watumishi mahali pa kazi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Bw. Mbwasi aliwasisitiza wajumbe kufanya kazi kwa utu, ushirikiano na uwajibikaji ili kuendelea kuimarisha utendaji wa taasisi pamoja na huduma zinazotolewa kwa wadau wake.
.hmwinyi
07/05/2026
Leo Mei 7, 2026, Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu Huduma kutoka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Bw. Thomas Mwita, amefungua kikao cha mafunzo kwa watumishi wa Bodi hiyo yaliyofanyika katika Hotel ya Morena, mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo watumishi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Mafunzo hayo yalihusu masuala ya HIV/AIDS na magonjwa yasiyoambukiza, maadili ya Utumishi wa Umma, kuzuia na kupambana na rushwa, afya ya akili, elimu ya fedha ,matumizi na utunzaji sahihi wa kumbukumbu na nyaraka.
Kupitia mafunzo hayo watumishi wamehimizwa kuzingatia maadili ya kazi, kulinda afya zao pamoja na kutumia elimu waliyoipata kuongeza tija katika utoaji wa huduma ndani ya taasisi.
.hmwinyi
07/05/2026
Maadhimisho ya Miaka 20 ya WRRB yanaendelea kuwakutanisha wadau muhimu wa maendeleo ya uchumi nchini.
Tunathamini ushiriki wa UTT AMIS .amis k**a mdhamini wa tukio hili muhimu.
π
17β19 Mei 2026
π Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), Dodoma
π¨ Kaulimbiu: Mfumo Imara, Uchumi Endelevu
07/05/2026
Ubora ni msingi wa maendeleo endelevu.
Tunafurahia kushiriki kwa Tanzania Bureau of Standards ( ) k**a exhibitor katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya WRRB.
π
17β19 Mei 2026
π Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), Dodoma
π¨ Kaulimbiu: Mfumo Imara, Uchumi Endelevu