Land Transport Regulatory Authority - LATRA
Official account for Land Transport Regulatory Authority (LATRA).
23/06/2026
WADAU WATEMBELEA BANDA LA LATRA KATIKA KILELE CHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, 2026.
Wadau mbalimbali wa usafiri ardhini wametembelea banda la LATRA katika Kilele cha Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na kupatiwa elimu kuhusu kazi, majukumu na huduma mbalimbali zinazotolewa na LATRA, Juni 23, 2026.
Maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni, 2026, yakiwa na kaulimbiu isemayo, “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa huduma Endelevu”
23/06/2026
CPA, Dkt. Habibu Juma Suluo, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) akiambatana na Bw. Christopher Philemon Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Serikalini - Wizara ya Uchukuzi, wametembelea Banda la LATRA Juni 22, 2026 lililopo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo wameshuhudia wadau mbalimbali wakipatiwa elimu kuhusu shughuli za udhibiti zinazotekelezwa na LATRA.
Aidha, CPA, Dkt. Suluo alipata wasaa wa kutembelea Taasisi mbalimbali zilizopo chini wa Wizara ya Uchukuzi ikiwemo banda la Wizara ya Uchukuzi, Shirika la Reli Tanzania (TRC), Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Kampuni ya Meli Tanzania pamoja na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), na kupatiwa elimu kuhusu kazi na majukumu ya taasisi hizo.
22/06/2026
Prof. Godius Kahyarara, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, ametembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Juni 22, 2026 lililopo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na kupokea maelezo kuhusu kazi ya kutoa elimu inayofanyika katika maonesho hayo.
Prof. Kahyarara, ameipongeza LATRA kwa ubunifu wa kuungalisha mifumo ya tiketi za treni ya kisasa SGR na mfumo mkuu wa utoaji tiketi za mtandao (Safari Tiketi) ambao umerahisisha upatikanaji wa tiketi za SGR kwa wananchi na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma ya usafiri wa treni nchini.
Maonesho hayo yenye kaulimbiu “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu” yanafanyika kuanzia Juni 16 hadi 23, 2026 viwanja vya Chinangali Park jijini, Dodoma.
22/06/2026
Bw. Juma Mkomi, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ametembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Juni 22, 2026 lililopo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na kushuhudia shughuli za Udhibiti zinazo tekelezwa na LATRA.
Bw. Mkomi, ameipongeza LATRA kwa kazi nzuri ya kutoa elimu katika maonesho hayo ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kero za usafiri wa ardhini, pia amesisitiza LATRA kuendelea kushiriki katika maonesho haya ili kuwezesha kuwafikia wadau ambao wanapatikana kwenye maonesho hayo.
Maonesho hayo yenye kaulimbiu “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu” yanafanyika kuanzia Juni 16 hadi 23, 2026 viwanja vya Chinangali Park jijini, Dodoma.
22/06/2026
Mhe. Regina Qwaray (Mb), Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ametembelea banda la Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Juni 22, 2026 lililopo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na kushuhudia shughuli za Udhibiti zinazo tekelezwa na LATRA.
Mhe. Qwaray, ameipongeza LATRA kwa kazi nzuri wanayoifanya ikiwemo kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA ambayo imewarahisishia upatikanaji wa huduma za usafiri ardhini kwa abiria na watumiaji wengine kupitia mifumo k**a vile Safari Tiketi mfumo jumuishi wa ukataji wa tiketi ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kero kwa abiria.
Aidha, Akitoa maelezo katika banda la LATRA, CPA, Dkt. Habibu Juma Suluo, Mkurugenzi Mkuu LATRA, amesema kuwa, kaulimbiu ya maadhimisho haya inayosema “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa huduma Endelevu” kaulimbiu hii LATRA inaiishi kwa vitendo na kuhakikisha huduma za LATRA zinakuwa endelevu wakati wote kwa kufuata viwango vya kimataifa vya utoaji huduma.
Maonesho hayo yanafanyika kuanzia Juni 16 hadi 23, 2026 viwanja vya Chinangali Park jijini, Dodoma.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Nkrumah Street, Near Clock Tower
Dar Es Salaam
3093
