23/06/2026
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano -
The Consumer Consultative Council of the Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA-CCC)
23/06/2026
22/06/2026
Kagera
TCRA CCC Yateta na Wanafunzi wa Chuo cha King Rumanyika Kagera.
Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Kagera imewasihi wanafunzi wa vyuo nchini kuifahamu vyema Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 ili kujua Haki na Wajibu walio nao.
Akizungumza na Wanachuo wa Chuo cha King Rumanyika kilichopo katika Kata ya Nshambya mkoani Kagera, Mwenyekiti wa Kamati ya Watumiaji Mkoa huo ndugu Prosper Mbakile amesema Vijana kuijua Sheria hiyo kutawaepusha na makosa ya mtandaoni wanayotenda pasi na kujua.
"Unakuta Kijana amemtukana mwenzie kwenye mtandao k**a vile Instagram au amemkashifu. miezi kadhaa imepita, kasahau, anashangaa kak**atwa, kumbe mwenzie alishtaki. Sasa, hivi ni vitu vidogo vidogo ambavyo unaweza kupuuza kumbe ni kosa la kimtandao! Jielimisheni Ndugu zangu!", amesema Mbakile.
Kamati hiyo ya Watumiaji Mkoa wa Kagera inaendelea na Kampeni ya kuelimisha makundi mbalimbali kuhusu matumizi sahihi ya Mawasiliano ikiwa ni Mkakati wa kuwafikia Watanzania Nchi nzima, unaoendeshwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano nchini (TCRA CCC) k**a hatua mojawapo ya kusaidia watumiaji kufahamu Sheria na Miongozo mbalimbali ambayo inasimamiwa matumizi sahihi na salama ya huduma za mawasiliano.
21/06/2026
Linda taarifa zako binafsi, usitoa taarifa zako binafsi bila kujiridhisha.
Shiriki katika kumlinda mtoto dhidi ya ukatili na udhalilishaji mtandaoni.
CHUKUA HATUA SASA!
16/06/2026
Tuwalinde Watoto dhidi ya Ukatili Mtandaoni.
CHUKUA HATUA SASA!
16/06/2026
Siku ya Mtoto wa Afrika, Juni 16 2026.
Mtoto ni Malezi; Msingi wa Familia Bora kwa Taifa Imara.
| Monday | 08:00 - 17:00 |
| Tuesday | 08:00 - 17:00 |
| Wednesday | 08:00 - 17:00 |
| Thursday | 08:00 - 17:00 |
| Friday | 08:00 - 17:00 |