Wow.... big up, huduma zipi nyingine ungependa zipatikane kwa kutumia Kitambulisho cha Taifa?
Tuambie kwenye comments.
National Identification Authority - NIDA
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa - NIDA
03/06/2026
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imechangia uzoefu wake katika mjadala wa kujenga Mfumo wa Mawasiliano ya Serikali wenye dira moja, sauti moja na uratibu wa pamoja kwenye "Dira2050", ikiwa ni sehemu ya Mkutano Mkuu wa Maafisa Mawasiliano wa Serikali unaofanyika jijini Mwanza.
Mkutano huo umefunguliwa rasmi tarehe 2 Juni 2026, na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mohamed Mtanda, na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO), Karim Meshaki, alieleza mipango ya chama hicho katika kuongeza weledi wa wanachama wake, kuimarisha mifumo ya uendeshaji wa shughuli za chama kupitia TEHAMA, pamoja na maandalizi ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa Makao Makuu ya TAGCO jijini Dodoma.
Katika mkutano huo, Sarah Reuben, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati - NIDA, alishiriki uzoefu wake katika sekta ya mawasiliano kupitia mada ya βOne Nation, One Vision: Building a Whole-of-Government Communication System for Vision 2050,β ambapo alisisitiza umuhimu wa taarifa sahihi, uratibu wa pamoja na mawasiliano ya Serikali yanayomfikia mwananchi kwa wakati na kwa lugha inayoeleweka.
Kupitia ushiriki huo, NIDA imeonesha dhamira yake ya kuendelea kuboresha mawasiliano ya kitaasisi katika kuelimisha wananchi kuhusu usajili, utambuzi na matumizi ya Kitambulisho cha Taifa k**a nyenzo muhimu ya kupata huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
29/05/2026
Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka 2026/2027
27/05/2026
Eid Al Adha Mubarak π
Tunawatakia watanzania wote na Eid yenye amani, furaha na baraka tele.
ππβ€οΈ
Waajiri na Wafanyakazi kuhakikishiwa usalama wao. Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Serikali kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi. Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
25/05/2026
Bungeni Leo π₯π₯
25/05/2026
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa wanaweza kufuatilia mubashara Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inayowasilishwa leo Bungeni.
Matangazo hayo yanapatikana kupitia ukurasa rasmi wa YouTube wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Tafadhali tumia kiunganishi kilichowekwa hapa kufuatilia.
https://www.youtube.com/live/5iGD8ZigXgQ?si=KpmJkr2fvpiUxAlw
Usikose kufuatilia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027, itakayosomwa tarehe 25 Mei, 2026.
Donβt miss the Budget Speech of the Ministry of Home Affairs for the Financial Year 2026/2027, to be delivered on 25 May, 2026.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Telephone
Website
Address
12324
Dar Es Salaam
