Maendeleo ya Jamii

Maendeleo ya Jamii

Share

Ukurasa rasmi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wanawake na Makundi Maalum

12/06/2026
Photos from Maendeleo ya Jamii's post 12/06/2026
Photos from Maendeleo ya Jamii's post 12/06/2026

TANZANIA YAENDELEA KUIMARISHA AJENDA YA WANAWAKE, AMANI NA USALAMA

Na WMJJWM Rome Italia

Tanzania imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuimarisha usawa wa kijinsia, amani na usalama kwa kushiriki katika Mkutano wa Nane wa Ngazi ya Juu wa Mtandao wa Kimataifa wa Nchi zinazotekeleza Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama (WPS) uliofanyika jijini Rome, Italia, Juni 8 hadi 10, 2026.

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Jinsia na Wanawake kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na Sekretarieti ya Mtandao wa Kimataifa wa WPS chini ya UN Women kwa ushirikiano na nchi ya Italia na Ufilipino ambazo kwa mwaka 2026 zilikuwa zikihudumu k**a Mwenyekiti na Mwenyekiti Mwenza wa mtandao huo umewakutanisha wawakilishi kutoka nchi zaidi 70 duniani, ulijadili mustakabali wa ajenda ya wanawake katika masuala ya amani na usalama.

Miongoni mwa mambo ya kipaumbele ni utekelezaji wa Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama katika kukabiliana na changamoto zinazoendelea za amani na usalama duniani. Washiriki walisisitiza umuhimu wa kuweka mkakati madhubuti unaozingatia matokeo ili kuhakikisha malengo ya ajenda hiyo yanafikiwa kwa ufanisi.

Aidha, mkutano huo ulijadili umuhimu wa kuongeza ushiriki kamili, sawa na salama wa wanawake katika michakato ya kuzuia migogoro, kutatua migogoro na kujenga amani. Viongozi mbalimbali walikubaliana kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika kujenga jamii zenye utulivu na maendeleo endelevu.

mkutano huo pia uliangazia changamoto mpya zinazohusiana na usalama, ikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi, uhamaji wa watu, maendeleo ya teknolojia za kidijitali pamoja na umuhimu wa kushirikisha vijana kupitia Ajenda ya Vijana, Amani na Usalama (YPS) ili kujenga kizazi chenye mchango chanya katika masuala ya amani.

Mazungumzo hayo yalijikita katika kuendeleza ajenda za maendeleo ya jamii, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake na makundi maalum pamoja na nafasi ya diplomasia katika kutangaza maslahi ya Tanzania kimataifa.

Mkutano huo umetoa fursa ya kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano utakaosaidia Tanzania kuendelea kunufaika

Photos from Maendeleo ya Jamii's post 11/06/2026

TANZANIA NA GIZ ZASAINI MAKUBALIANO YA KUIMARISHA USHIRIKISHWAJI WA WANAWAKE KATIKA TEKNOLOJIA ZA KIDIJITALI.

Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam WMJJWM

Serikali ya Tanzania na Ujerumani zimesaini Makubaliano ya Utekelezaji wa Mradi wa Kituo cha Mabadiliko ya Kidijitali Tanzania (Digital Transformation Centre – DTC Tanzania), utakayochochea ushiriki wa wanawake na wasichana katika uchumi wa kidijitali kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini baina ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) iliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 11, 2026, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Bw. Badru Alburnoor amesema makubaliano hayo yanafungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya nchi ya Tanzania na Ujerumani katika kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata fursa sawa za kushiriki na kunufaika na maendeleo ya teknolojia za kidijitali.

Amesema mradi huo unaendana kikamilifu na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Jinsia na Wanawake ya mwaka 2023, Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto pamoja na Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali wa mwaka 2024–2034.

“Teknolojia za kidijitali zimekuwa nyenzo muhimu katika kubadilisha namna wananchi wanavyojifunza, kufanya kazi, kupata huduma na kushiriki katika shughuli za maendeleo. Serikali inaona umuhimu wa kuhakikisha wanawake na wasichana hawabaki nyuma katika mabadiliko haya, bali wanakuwa sehemu ya nguvu kazi na wabunifu wa teknolojia zinazochochea maendeleo ya taifa,” amesema Alburnoor.
Ameongeza kuwa kabla ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Wizara kwa kushirikiana na GIZ tayari imefanikiwa kutekeleza programu mbalimbali zilizolenga kukuza ushiriki wa wanawake katika sekta ya teknolojia, kuimarisha ujuzi wa kidijitali na kuhamasisha ubunifu unaotumia teknolojia katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi.

Kwa mujibu wa Alburnoor, Mradi wa DTC Tanzania unalenga kuendeleza suluhisho za kidijitali zinazobuniwa ndani ya nchi huku ukijenga mazingira jumuishi ya ushiriki katika uchumi.

Photos from Maendeleo ya Jamii's post 11/06/2026

TANZANIA YAONGOZA MJADALA WA KIMATAIFA KUHUSU UIMARISHAJI WA HUDUMA NA MSAADA KWA WATU WENYE ULEMAVU

Na mwandishi wetu- New York, Marekani.

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Balozi Togolani Mavura, ameongoza mjadala wa ngazi ya juu katika Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (COSP19), uliojikita katika mada ndogo ya “Jamii Imara: Kuimarisha Mifumo ya Huduma na Msaada ili Kuhakikisha Uwezeshaji, Uhuru na Kujitegemea kwa Watu Wote Wenye Ulemavu.”

Akifungua mjadala huo, Mhe. Balozi Togolani amesema huduma na mifumo ya msaada ni msingi muhimu wa ustawi wa watu binafsi, jamii na uchumi kwa ujumla, huku akisisitiza kuwa utekelezaji wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu umeleta mafanikio makubwa duniani katika kipindi cha miaka 20 tangu kupitishwa kwake.

"licha ya hatua zilizofikiwa, bado watu wengi wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto za kupata huduma na msaada unaokidhi mahitaji yao, hali iliyodhihirika zaidi wakati wa janga la UVIKO-19 ambapo mifumo mingi ya huduma ilionekana kutokuwa imara na jumuishi vya kutosha hivyo ni muhimu kuimarisha huduma za usaidizi binafsi, huduma za urekebishaji na uendelezaji uwezo, vifaa saidizi, mifumo ya hifadhi ya jamii pamoja na huduma za kijamii zinazotolewa katika ngazi ya jamii katika kuwawezesha watu wenye ulemavu kufanya maamuzi yao wenyewe, kuishi kwa kujitegemea na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii, kiuchumi na kisiasa."Alisema Mhe. Balozi Togolani.

Kwa upande wake Afisa Sheria kutoka kitengo cha Watu Wenye Ulemavu,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Bw. Jacob C. Mwinula, akiwasilisha uzoefu wa Tanzania katika kuimarisha mifumo ya huduma na msaada kwa watu wenye ulemavu wakati wa mjadala (Roundtable Discussion) ameeleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuimarisha ujumuishaji, kujitegemea na ushiriki wa watu wenye ulemavu kupitia sera, sheria, mifumo ya hifadhi ya jamii, huduma za afya, elimu jumuishi na uwezeshaji wa kiuchumi.

10/06/2026

SERIKALI KUCHUNGUZA IWAPO KUNA UJIO WA TAMASHA LINALOTAJWA KUTOZINGATIA MAADILI YA KITANZANIA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mheshimiwa Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Serikali itafuatilia na kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli kuhusu taarifa za uwepo wa tamasha linalodaiwa kuwa na maudhui yasiyozingatia maadili, mila na desturi za Kitanzania.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema Serikali itaendelea kusimamia, kulinda na kuimarisha maadili ya jamii kwa kushirikiana na Wizara, taasisi za Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wadau mbalimbali ili kuhakikisha shughuli zote zinazofanyika nchini zinazingatia sheria, tamaduni na maadili ya Taifa. Amesisitiza kuwa hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mtu, kikundi au tukio lolote litakalobainika kukiuka maadili na misingi ya Kitanzania.

Dkt. Gwajima amesema hayo Juni 10, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Katavi, Mheshimiwa Thomas Kamala, aliyetaka kufahamu iwapo Serikali inafahamu kuhusu taarifa za ujio wa tamasha hilo na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha maadili ya Kitanzania yanaendelea kulindwa na kuenziwa.

10/06/2026

SERIKALI KUHAMASISHA UTEKELEZAJI WA MIKAKATI YA USAWA WA KIJINSIA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mheshimiwa Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Wizara ina mpango wa kuwateua Mbunge wa Kigoma Mjini, Mheshimiwa Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo), pamoja na Mbunge wa Jimbo la Katavi Mheshimiwa Thomas Kampala kuwa Mabalozi wa Wanaume nchini.

Dkt. Gwajima amesema kupitia uwezo wao wa kuwasilisha hoja na kuhamasisha wanaume, wataweza kukusanya na kuwasilisha maoni, changamoto na hoja zinazowagusa wanaume ili kusaidia kuboresha utekelezaji wa mikakati ya usawa wa kijinsia na ustawi wa familia.

Dkt. Gwajima. Ametoa kauli hiyo Juni 10, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Fatma Rembo

Aidha, Dkt. Gwajima amesema ushirikishwaji wa wanaume katika ajenda za usawa wa kijinsia ni muhimu ili kujenga jamii yenye usawa, maelewano na maendeleo jumuishi kwa wote.

10/06/2026

WAZIRI DKT. GWAJIMA AELEZA MIKAKATI YA SERIKALI KUIMARISHA MALEZI NA ULINZI WA WATOTO KUKABILIANA NA MMOMONYOKO WA MAADILI

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mheshimiwa Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Serikali kupitia Wizara hiyo inaendelea inatekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha malezi, makuzi na ulinzi wa watoto pamoja na kukabiliana na mmomonyoko wa maadili nchini.

Dkt. Gwajima amesema mikakati hiyo ni pamoja na utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ya miaka mitano kuanzia mwaka 2021/22, Programu Jumuishi ya Taifa ya Kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana Balehe wenye umri wa miaka 9 hadi 19, pamoja na Mpango wa Pili wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA II) wa mwaka 2024/25.

Aidha, amesema Serikali imezindua Mkakati wa Taifa wa Miaka 10 wa Kukabiliana na Mmomonyoko wa Maadili kuanzia mwaka 2026/27, imeunda Kamati ya Taifa ya Ushauri kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni na imeanza kujadili hatua za kuchuja maudhui yasiyofaa mtandaoni pamoja na uwezekano wa kuwa na laini maalum za huduma kwa watoto.

Dkt. Gwajima ameeleza kuwa utekelezaji wa mikakati hiyo unahusisha sekta mbalimbali kuanzia ngazi za Serikali za Mitaa hadi Taifa. Amesema Serikali inaendelea na mchakato wa kuunda Kamati za Maadili katika ngazi za kata, halmashauri, wilaya na mikoa ili kuimarisha ushirikiano wa wadau katika kulinda maadili, usalama na ustawi wa watoto.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo Juni 10, 2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum kupitia Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Catherine Joachim.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


573
Dodoma