MAFUNZO YA NEST YAWAJENGEA UWEZO MAAFISA UDHIBITI UBORA WA SHULE NCHINI.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
This is an official FACEBOOK PAGE for Ministry of Education, Science and Technology in Tanzania
Serikali kupitia Samia Scholarship imetekeleza azma ya kuwekeza katika nyanja ya elimu, sayansi, uhandisi, akili Unde na teknolojia za viwanda.
Samia Scholarship ni fursa kwa vijana kupata umahiri katika sayansi na Teknolojia ili kushindana katika dunia ya sasa yenye maendeleo makubwa ya teknolojia.
12/06/2026
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Katare Bugwesa, amebainisha kuwa kiunzi hicho kinalenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika maamuzi, kuimarisha maendeleo yao kitaaluma na kujumuisha masuala ya kijinsia katika tafiti na bunifu.
Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Prof. Ladislaus Mnyone, amesema ushiriki wa makundi yote ni muhimu ili juhudi za nchi ziwe na matokeo ya pamoja na kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa haraka zaidi.
PROF. NOMBO ASISITIZA USAWA WA KIJINSIA KATIKA UTAFITI
12/06/2026
PROF. NOMBO ASISITIZA USAWA WA KIJINSIA KATIKA UTAFITI
Serikali imeendelea kusisitiza ushiriki jumuishi wa wanawake, vijana na makundi yenye mahitaji maalum katika utafiti, sayansi, teknolojia na ubunifu ili kuongeza mchango wao katika maendeleo ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa Juni 12, 2026 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, wakati wa ufunguzi wa Warsha ya kuwajengea uwezo Wadau kuhusu Utekelezaji wa Kiunzi cha Kitaifa cha Usawa na Haki za Kijinsia katika Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU).
Ameeleza kuwa kwa sasa wanawake ni takribani asilimia 36 ya watafiti nchini, huku wasichana wakichangia zaidi ya asilimia 45 ya wanafunzi wapya wa masomo ya STEM vyuoni katika mwaka wa fedha 2023/24.
Ameongeza kuwa vijana walio chini ya miaka 35 wamechangia karibu asilimia 40 ya miradi iliyoidhinishwa na COSTECH katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Katibu Mkuu Nombo amesisitiza kuwa taasisi za utafiti na ubunifu zinapaswa kutumia kikamilifu kiunzi hicho katika sera, mipango na bajeti zao ili kuhakikisha matokeo ya tafiti na bunifu yananufaisha wananchi wote na kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa.
“Nchi yetu imeendelea kutambulika kimataifa katika kuisimamia na kuendeleza usawa wa kijinsia chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye alichaguliwa kuwa Kinara wa kuendeleza ajenda hii, sisi k**a wadau wa STU tunapaswa kuunga mkono maono haya na kuhakikisha yanazingatiwa katika shughuli zote za maendeleo ya Taifa" amesema Prof. Nombo.
WATHIBITI UBORA WA SHULE WANOLEWA MATUMIZI YA NEST
11/06/2026
WATHIBITI UBORA WA SHULE WAASWA KUSIMAMIA KWA WELEDI MATUMIZI YA NEST
Wathibiti Ubora wa Shule nchini wametakiwa kusimamia kwa weledi matumizi ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) ili kuhakikisha manunuzi yote ya Serikali yanafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.
Rai hiyo imetolewa Juni 11, 2026 jijini Arusha na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Fredrick Salukele, akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, katika ufunguzi wa mafunzo kuhusu matumizi ya Mfumo huo.
Dkt. Salukele amesema mafunzo hayo yatawawezesha washiriki kutumia mfumo huo kwa ufanisi katika usimamizi wa fedha za uchangiaji, ununuzi wa bidhaa na huduma mbalimbali pamoja na malipo ya shughuli za tathmini za shule.
Amewasisitiza washiriki kusimamia kwa ufanisi rasilimali zilizopo, ikiwemo rasilimali watu na miundombinu, sambamba na kuimarisha huduma bora za elimu.
Aidha, Dkt. Salukele amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri na Wathibiti Ubora wa Shule kuhakikisha taasisi za elimu zinazingatia taratibu zote za uendeshaji ikiwemo masuala ya malazi, chakula na usalama wa wanafunzi.
Naye, Miurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule kutoka Wizara hiyo Dkt. Ephrahim Simbeye amesisitiza uzingatiaji wa miongozo ya elimu, akitaka kukomeshwa kwa adhabu zisizokubalika na kuhakikisha kuna mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi.
Nao baadhi ya Maafisa Wathibiti Ubora wa Shulewalioshiriki wakiwemo Afisa Lilian Kasenga Mthibiti Ubora kutoka Manispaa ya Temeke pamoja na Afisa Emmanuel Hangaya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, wametaja mbinu wanazotumia kufikia malengo huku wakisema mafunzo hayo yatakwenda kuwaongezea ufanisi kazini.
11/06/2026
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Website
Address
Mji Wa Serikali Mtumba/Mtaa Wa Afya S. L. P 10
Dodoma
40479DODOMA
Opening Hours
| Monday | 02:00 - 15:30 |
| Tuesday | 02:00 - 21:30 |
| Wednesday | 02:00 - 21:30 |
| Thursday | 02:00 - 21:30 |
| Friday | 02:00 - 09:30 |
