Duwasatz

Duwasatz

Share

Sambamba na hayo DUWASA pia inatoa huduma ya maji bure kwa watu wasiojiweza.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Mjini Dodoma-DUWASA inatoa huduma ya usambazaji wa maji safi pamoja na uondoshaji wa majitaka ikiwa ni usafi wa mazingira Jijini Dodoma.

Photos from Duwasatz's post 08/06/2026

DODOMA YAKABIDHI MWENGE WA UHURU MOROGORO

-Mradi wa Majisafi Nala miongoni wa miradi iliyozinduliwa na Mwenge.

​Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Heri James amekabidhi rasmi Mwenge wa Uhuru Kitaifa wa mwaka 2026 kwa uongozi wa Mkoa wa Morogoro, baada ya kumaliza mbio zake mkoani Dodoma ambapo ulikagua, uliweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

​Katika mbio hizo mkoani Dodoma, miongoni mwa miradi mikubwa iliyomulikwa na kuzinduliwa ni Mradi wa Majisafi wa Nala, ambao ulizinduliwa rasmi Juni 1, 2026. Mradi huo unatajwa kuwa mkombozi mkubwa wa upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi wa eneo hilo na maeneo jirani.

​Katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Wilayani Gairo, mkoa wa Morogoro, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Mhandisi Bernard Rugayi, imeshiriki kikamilifu tukio hilo muhimu ambalo linaashiria mafanikio makubwa katika usimamizi wa miradi ya kimkakati ya maji mkoani humo.

Photos from Duwasatz's post 06/06/2026

CCM DODOMA YAIPONGEZA DUWASA KWA MAPINDUZI YA MAJI, YALENGA ASILIMIA 100 IFIKAPO 2030

​Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma kimeipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa kasi kubwa na ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maji, hatua inayotajwa kuwatoa wananchi wengi katika kero ya muda mrefu ya uhaba wa maji.

​Pongezi hizo zimetolewa leo Juni 6, 2026 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Ndugu Jawadu Bakilana, alipotembelea na kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali ya maji katika maeneo ya Nala, Zuzu, na Nzuguni jijini Dodoma.

​Akiwa katika mradi wa maji wa Nzuguni, Ndugu Bakilana ameeleza kuridhishwa kwake na viwango vya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo imekuwa mkombozi mkubwa kwa jamii inayozunguka maeneo hayo na Jiji la Dodoma kwa ujumla.

​Ndugu Bakilana amebainisha kuwa, licha ya changamoto za upatikanaji wa maji zinazotokana na ongezeko kubwa la watu ukuaji na wa kasi wa jiji la Dodoma, jitihada zinazofanywa na DUWASA zimesaidia kufanikisha upatikanaji wa maji kwa asilimia 91 kwa Jiji la Dodoma.

​"Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika sekta ya maji hapa Dodoma unaenda vizuri sana na kwa kasi ya kuridhisha. Hali ya upatikanaji wa maji kwa sasa imefikia asilimia 91 katika Jiji letu. Hili ni dhihirisho la kusudio la dhati la CCM na Serikali yake kuhakikisha tunamaliza kabisa kero ya maji, ambapo lengo letu kuu ni kufikia asilimia 100 ya upatikanaji wa maji ifikapo mwaka 2030," alisema Ndugu Bakilana.

​Ziara hiyo ya ukaguzi ni sehemu ya mikakati ya CCM Mkoa wa Dodoma ya kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayolenga kuboresha maisha ya wananchi na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kulingana na ahadi za chama Tawala.

​Kupitia ziara hiyo, CCM imetoa wito kwa DUWASA kuendelea kudumisha kasi hiyo na kuwataka wananchi kuilinda miradi hiyo ya maji ili iweze kudumu na kuleta tija iliyokusudiwa kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.

Photos from Duwasatz's post 05/06/2026

*​Makamu wa Rais, Balozi Nchimbi aagiza Miradi ya Maji Kulinda Ardhi Oevu*

​Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameiagiza Wizara ya Maji kuhakikisha inatekeleza miradi yake yote kwa kuzingatia uhifadhi na ulinzi wa ardhi oevu nchini.

​Balozi Nchimbi ametoa agizo hilo leo Juni 5, 2026, jijini Dodoma, wakati akimwakilisha Rais katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

​Akizungumza katika maadhimisho hayo, Makamu wa Rais amesisitiza kuwa ardhi oevu ndio muhimili mkuu wa utunzwaji wa mazingira na vyanzo vya maji, hivyo ni lazima ilindwe kikamilifu dhidi ya uharibifu.

​"Hadi kufikia mwaka 2050, Tanzania inakadiriwa kuwa na wananchi zaidi ya milioni 100. Hivyo, utunzwaji wa ardhi oevu utasaidia kuendeleza vyanzo vya maji na kupunguza upungufu wa maji uliopo nchini kwa sasa na miaka ijayo," amesema Balozi Nchimbi.

​Katika hatua nyingine, kiongozi huyo amewataka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha wanazalisha miche ya miti ya kutosha ili ipandwe kwenye maeneo mbalimbali nchini, kwa lengo la kukijanisha taifa na kulinda vyanzo vya maji.

​Maadhimisho haya ya Siku ya Mazingira Duniani kwa mwaka huu yamehitimishwa na Makamu wa Rais yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo: “Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania,” ambapo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imeshiriki kikamilifu katika maonesho hayo kuonesha mchango wake wa utunzaji mazingira.

Photos from Duwasatz's post 05/06/2026
Photos from Duwasatz's post 04/06/2026

*WIKI YA MAZINGIRA: DUWASA YAWAFIKIA WANAFUNZI ELIMU YA UTUNZAJI VYANZO VYA MAJI*

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imetoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na matumizi sahihi ya mtandao wa majitaka kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege jijini hapa, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Mazingira Duniani.

​Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo, Afisa Mwandamizi wa Mazingira kutoka DUWASA, Bi. Maria Holela, amewahimiza wanafunzi hao kuwa mabalozi wema kwa kushirikiana na wazazi wao kulinda mazingira, hatua itakayosaidia kukabili mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaathiri upatikanaji wa huduma endelevu ya maji.

​Lengo kuu la kutoa elimu hiyo shuleni hapo ni kujenga, kuongeza na kurithisha uelewa wa masuala ya utunzaji wa mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

​Mbali na utunzaji wa mazingira, Bi. Holela amewaeleza wanafunzi hao umuhimu wa kutoa taarifa mapema kwa Mamlaka pindi wanapokutana na changamoto za miundombinu, ikiwemo mabomba ya majisafi au majitaka yanayovuja au kumwaga maji ovyo mitaani.

​Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Kitaifa kwa mwaka huu yanafanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma, yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo: “Dira 2030; Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.”

Photos from Duwasatz's post 04/06/2026

*​Naibu Waziri Dkt. Mk**a Aipongeza DUWASA kwa Kasi ya Huduma kwa Wateja*

​Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Switbert Mk**a (Mb), ameimwagia sifa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa ufanisi na kasi kubwa ya kuwahudumia wateja wake jijini hapa.

​Pongezi hizo amezitoa leo alipotembelea banda la Wizara ya Maji na Taasisi zake katika Maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Dkt. Mk**a amebainisha kuwa huduma bora na za haraka ni kielelezo cha weledi katika utekelezaji wa majukumu ya serikali kwa wananchi.

​Akiwa katika banda hilo, Mheshimiwa Mk**a alipata fursa ya kujionee miradi mbalimbali na teknolojia za kisasa zinazotumiwa na Sekta ya Maji.

Alieleza kuridhishwa kwake na namna Taasisi hizo zinavyotumia ubunifu kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama, pamoja na mifumo ya usafi wa mazingira nchini.

​"Nimeridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Maji pamoja na taasisi zake. Ni wazi kuwa kuna jitihada za makusudi kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa wakati," alisema Dkt. Mk**a.

​Aidha, Naibu Waziri alisisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi za kulinda vyanzo vya maji na rasilimali za mazingira, akibainisha kuwa uhifadhi wa sasa ndio utakaohakikisha usalama wa vizazi vijavyo.

"​Maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu inayosemayo: Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania, ambayo inahimiza kila mdau na mwananchi kuchukua hatua madhubuti za kurejesha uasili wa mazingira." Amesema Dkt. Mk**a.

​DUWASA, ikiwa ni moja ya Taasisi zilizoshiriki maonyesho hayo, imeendelea kuonyesha mikakati yake ya kuboresha huduma za majitaka na usambazaji wa maji katika Mji wa Serikali, huku ikizingatia utunzaji wa mazingira k**a sehemu ya mpango mkakati wake wa huduma.

​Maonyesho haya ya Wiki ya Mazingira Duniani 2026 yanaendelea kukutanisha wadau mbalimbali jijini Dodoma, yakiwa na lengo la kutoa elimu na kuhamasisha matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira.

Photos from Duwasatz's post 03/06/2026

DUWASA yashiriki Maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani yanaendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Photos from Duwasatz's post 01/06/2026

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI WA MAJISAFI, NALA - DODOMA

Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Leo Juni Mosi, 2026 Umezindua Mradi wa Majisafi wa Nala Jijini Dodoma unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA).

Akizungumza na Wananchi baada ya kuzindua mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Wazo Michael Mwang’onda amesema mradi huo umekidhi vigezo vya utekelezaji wake.

Ndugu Mwang’onda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa majisafi ambao umemtua mama ndoo kichwani.

Mradi wa Majisafi Nala tayari unahudumia wakazi zaidi ya 5,188 katika maeneo ya Nala Center, Segu Juu, Chihoni na Kiwanda cha Mbolea cha Nala cha Itracom.

27/05/2026
Photos from Duwasatz's post 09/05/2026

SERIKALI KUMALIZA KERO YA MAJI KIBAIGWA - KONGWA

Serikali imewahakikishia wakazi wa Kata ya Kibaigwa, Wilayani Kongwa, kumalizika kwa changamoto ya upatikanaji wa majisafi, kufuatia mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kununua mitambo ya kisasa ya kuchimbia visima kwa kila mkoa nchini.

​Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), wakati akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye stendi ya mabasi Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa Mei 08, 2026.

​Akifafanua jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya maji, Dkt. Nchemba alibainisha kuwa hatua ya awali ya upatikanaji wa mitambo imekamilika, na sasa Serikali inaelekeza nguvu kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa.

​"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshakamilisha ununuzi wa mitambo ya kuchimbia visima kwa kila mkoa. Hatua inayofuata sasa ni kutenga Bajeti mahususi ya kununua vifaa na kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya maji itakayomaliza kero hii kwa wananchi wa Kibaigwa na maeneo ya jirani," alisema Dkt. Nchemba.

​Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph, ameshiriki kikamilifu kuhakikisha maelekezo ya Serikali yanatekelezwa kwa manufaa ya Wananchi wa Kibaigwa.

​Waziri Mkuu yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili katika Wilaya za Kongwa (Kibaigwa) na Mpwapwa. Lengo kuu la ziara hiyo ni kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Salmin
Dodoma