05/06/2026
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga
Ukurasa rasmi wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga (Waga Wildlife Management Area)
05/06/2026
04/06/2026
KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI 2026.
Tarehe 03 Juni 2026, Menejimenti ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA kwa kushirikiana na walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi nyakadete , watumishi wa Zahanati ya Kijiji cha Nyakadete pamoja na wananchi wa kijiji hicho, walishiriki zoezi la usafi wa mazingira na upandaji wa miti katika eneo la zahanati hiyo.
Shughuli hiyo ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, yenye lengo la kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kushiriki kikamilifu katika juhudi za uhifadhi.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, Katibu wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA, John Samweli Mbulu, aliwahimiza wanafunzi kuwa mabalozi wa mazingira kwa kutunza miti iliyopandwa na kuendeleza utamaduni wa usafi wa mazingira katika shule na jamii zinazowazunguka.
04/06/2026
20/05/2026
Tarehe 19 Mei 2026, Menejimenti ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA kwa kushirikiana na shirika la Honeyguide Foundation ilifanya kikao maalum na wajumbe wa Kamati Tendaji kwa lengo la kupitia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za jumuiya.
Kikao hicho kilijadili maendeleo ya kazi zilizotekelezwa, changamoto zilizojitokeza pamoja na uhakiki wa nyaraka muhimu za jumuiya ikiwemo katiba, usajili, sheria ndogo, mikataba na MoU mbalimbali.
Aidha, shirika la Honeyguide Foundation ilisisitiza umuhimu wa kuweka nyaraka katika mfumo wa kidijitali ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kuimarisha uwazi katika utendaji.
Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori WAGA inatoa shukrani za dhati kwa Honeyguide Foundation kwa ushirikiano na mchango wake katika kuimarisha utawala bora na maendeleo ya jumuiya.
,
11/05/2026
Kuanzia tarehe 04 hadi 08 Mei 2026, Menejimenti ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA, kwa kushirikiana na Kamitei Foundation, imefanikiwa kugawa vitabu vya kufundishia pamoja na vifaa mbalimbali vya elimu kwa shule za msingi zilizopo katika maeneo yetu.
Shule zilizonufaika na zoezi hili ni Mahuninga, Kisilwa, Ihanzutwa, Igomaa, Nyamakuyu, Nyakadete, Mahango, Iheha, Nyakazombe, Magigiwe, Mapogoro A, Mapogoro B, Mlungu pamoja na Msagaji Mpya.
Katika zoezi hilo, zaidi ya vitabu 1,547 viligawiwa sambamba na vifaa vya kufundishia na kujifunzia zaidi ya 4,128, vikiwemo atlas, kamusi, manila paper, paper plates, gundi, cartons za box za chaki chaki pamoja na vifaa vingine muhimu vya elimu.
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA inaamini kuwa elimu bora ni msingi muhimu katika kujenga jamii yenye uelewa wa uhifadhi wa mazingira na rasilimali za asili kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Kupitia msaada huu, tunalenga kuchochea maendeleo ya elimu sambamba na kuimarisha ushiriki wa jamii katika masuala ya uhifadhi.
Walimu waliopokea vifaa hivyo walitoa shukrani zao za dhati na kuahidi kuwasilisha taarifa hizi kwa Afisa Elimu wa Wilaya ili kuthibitisha mchango mkubwa uliotolewa katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Kwa niaba ya uongozi wa WAGA, tunatoa shukrani za dhati kwa Kamitei Foundation pamoja na wadau wengine wote waliofanikisha zoezi hili muhimu la kusaidia elimu kwa watoto wetu na jamii kwa ujumla.
08/05/2026
Tarehe 5 Mei 2026, Menejimenti ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA ilifanya kikao na kampuni ya carbon Tanzania Mjini Iringa kwa lengo la kujadili utekelezaji wa mradi wa biashara ya hewa ukaa ndani ya maeneo ya hifadhi.
Kikao hicho kilifanyika katika mazingira mazuri na yenye tija, kikilenga kuimarisha usimamizi endelevu wa rasilimali za asili pamoja na kutathmini fursa za uwekezaji zitakazonufaisha jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi.
Majadiliano yalijikita katika namna bora ya kuendeleza mradi huo kwa kuzingatia misingi ya uhifadhi endelevu, ushirikishwaji wa jamii, na manufaa ya kiuchumi pamoja na kimazingira yatokanayo na biashara ya hewa ukaa.
Wadau mbalimbali walihudhuria kikao hicho wakiwemo , Muungano wa Jumuiya za Hifadhi za Jamii (CWMAC), Honeyguide foundation,STEP pamoja na mkuu wa idara ya wanyamapori kutoka Wilaya ya Iringa na mufindi
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori WAGA inapenda kutoa shukrani za dhati kwa Carbon Tanzania na wadau wote kwa ushirikiano na mchango wao katika kufanikisha kikao hicho, huku ikiendelea kuhimiza ushirikiano wa pamoja katika uhifadhi endelevu wa mazingira na maendeleo ya jamii.
05/04/2026
Heri ya Sikukuu ya Pasaka! 🐣🌿
Kutoka Waga WMA, tunawatakia Pasaka yenye furaha, amani na matumaini mapya. 💚✨
🌳
04/04/2026
Mnamo tarehe 1 april 2026 Menejimenti ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga ilifanikiwa kufanya kikao cha kikatiba na wajumbe wa Baraza la Jumuiya.
Katika kikao hicho, masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na;Mafanikio yaliyopatikana kupitia ushiriki wa Ranger Challenge 2025/2026, Utekelezaji wa ahadi za mwekezaji, Shughuli zilizotekelezwa katika kipindi cha Januari hadi Machi, Taarifa za fedha (mapato na matumizi)
Wajumbe wa Baraza walipongeza juhudi zote zilizofanyika na maendeleo yaliyopatikana. Aidha, waliomba kuondoka na nakala za taarifa za mapato na matumizi ili waweze kuziwasilisha na kuzichambua katika mikutano yao ya vijiji.
, , , ,
04/04/2026
Mnamo tarehe 1 april 2026 Menejimenti ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Waga ilifanikiwa kufanya kikao cha kikatiba na wajumbe wa Baraza la Jumuiya.
Katika kikao hicho, masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na;Mafanikio yaliyopatikana kupitia ushiriki wa Ranger Challenge 2025/2026, Utekelezaji wa ahadi za mwekezaji, Shughuli zilizotekelezwa katika kipindi cha Januari hadi Machi, Taarifa za fedha (mapato na matumizi)
Wajumbe wa Baraza walipongeza juhudi zote zilizofanyika na maendeleo yaliyopatikana. Aidha, waliomba kuondoka na nakala za taarifa za mapato na matumizi ili waweze kuziwasilisha na kuzichambua katika mikutano yao ya vijiji. , , ,
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Website
Address
Iringa
P.O.BOX223,MAFINGA-MUFINDI
Opening Hours
| Monday | 08:30 - 17:00 |
| Tuesday | 08:30 - 17:00 |
| Wednesday | 08:30 - 17:00 |
| Thursday | 08:30 - 17:00 |
| Friday | 08:30 - 17:00 |
| Saturday | 08:30 - 17:00 |
| Sunday | 08:00 - 17:00 |
