Tanzania Forestry Research Institute

Tanzania Forestry Research Institute

Share

Tanzania Forestry Research Institute (TAFORI) was established by Act No. 5 of 1980.

27/05/2026

🌙🐐

23/05/2026

🐝🍯Zijue sifa za kufuga nyuki kibiashara!

🐝 *Mdahalo wa Biashara kwa Biashara (B2B)? Ep.1*

Tazama video hii ya Mtafiti wa Ufugaji Nyuki- TAFORI Bw. Stansslaus Lukiko akitoa elimu kwa wadau na wawekezaji wa sekta hiyo kuhusu *fursa na namna ya kufuga nyuki kibiashara* kwa kuzingatia matokeo ya tafiti za hivi karibuni za TAFORI.

📍 *Mdahalo huu ulifanyika Viwanja vya Kumbukumbu ya Vita, Tabora.*

23/05/2026

Je wajua kuwa kuna makundi mavivu ya nyuki?Unasimamizi mzuri wa manzuki yako? Ep.2.

23/05/2026

🐝 *JE WEWE UNAFUGA NYUKI KIBIASHARA?? Mdahalo wa Biashara kwa Biashara (B2B)?* Ep.02

Photos from Tanzania Forestry Research Institute's post 23/05/2026

THAMANI YA MAZAO YA NYUKI YAONGEZEKA, MAUZO YA ASALI YAFIKIA SH. BILIONI 19.2

TABORA, Mei 22, 2026, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema sekta ya ufugaji nyuki inaendelea kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa huku thamani ya mazao ya nyuki ikiendelea kukua kutokana na ongezeko la uzalishaji na mauzo ya asali ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Kumbukumbu ya Vita mkoani Tabora, Dkt. Kijaji alisema ushiriki wa sekta binafsi unaendelea kuwa mhimili muhimu katika kuifanya Tanzania kuendelea kung’ara kimataifa katika sekta ya ufugaji nyuki.

Alisema Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji, wadau wa maendeleo na sekta binafsi ili kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao ya nyuki, hatua itakayochochea ajira, kuongeza kipato cha wananchi na kuimarisha mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa Taifa.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, mwaka 2025 Tanzania iliuza nje tani 1,596.8 za asali ikilinganishwa na tani 951 mwaka 2024, huku thamani ya mauzo hayo ikifikia Shilingi bilioni 19.2.

“Ndugu zangu, tunaona jinsi zao hili litokanalo na nyuki linavyoendelea kuongeza thamani kwa Taifa. Mbali na Tanzania kushika nafasi ya pili Afrika katika uzalishaji wa asali, thamani ya asali imepanda hadi kufikia Sh bilioni 19.2 mwaka jana. Hii ni hatua kubwa katika kuthamini mchango wa sekta ya nyuki,” alisema Dkt. Kijaji.

Aidha, alisema sekta ya ufugaji nyuki inakadiriwa kuajiri takribani watu milioni mbili nchini na imeendelea kuwa moja ya sekta zenye mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi.

Katika kuendeleza sekta hiyo, Dkt. Kijaji alisema Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa “Achia Shoka, Tundika Mzinga” unaolenga kuongeza uzalishaji, ajira na ushiriki wa vijana katika shughuli za ufugaji nyuki.

Aliongeza kuwa Tanzania imeendelea kushika nafasi ya kwanza kwa uzalishaji wa asali katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini, ikiwa ya pili barani Afrika na ya 14 duniani.

Aidha, maadhimisho ya mwaka 2026 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Uhifadhi wa Nyuki kwa Ustawi”, inayolenga kuhimiza uhifadhi wa mazingira, ustawi wa nyuki na maendeleo endelevu.

22/05/2026

“NITOE RAI KWA WOTE AMBAO MMEKABIDHIWA DHAMANA YA KUSIMAMIA MIUNDOMBINU YA UFUGAJI NYUKI HAKIKISHENI MNAITUNZA NA ILETE TIJA ILIYOKUSUDIWA KWA WANANCHI NA TAIFA KWA UJUMLA” : MHE. DKT ASHATU KIJAJI.

Photos from Tanzania Forestry Research Institute's post 22/05/2026

SERIKALI YAKAMILISHA UTHIBITISHAJI WA VIGEZO VYA UTEUZI WA VIJIJI NA MAENEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUJENGA UHIMILIVU DHIDI YA MABADILIKO YA TABIANCHI KIGOMA

Kasulu, Kigoma | Mei 20, 2026 – Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), kwa kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) kupitia ufadhili wa Serikali ya Tanzania na Green Climate Fund (GCF), imekamilisha hatua muhimu ya kuthibitisha vigezo vya uteuzi wa vijiji, maeneo ya utekelezaji na wanufaika wa Mradi wa Kujenga Uhimilivu dhidi ya Athari za Mabadiliko ya Tabianchi katika Mkoa wa Kigoma.

Hatua hiyo itasaidia kuongoza utekelezaji wa shughuli za Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (CBFM), upandaji miti (Afforestation) na kilimo misitu (Agroforestry) katika wilaya za Kasulu, Kakonko na Kibondo.

Uthibitishaji huo ulifanyika kupitia warsha iliyofanyika Chuo cha Ualimu Kasulu iliyowakutanisha wataalamu wa sekta za misitu, kilimo na ardhi kutoka wilaya husika, watendaji kutoka vijiji 22 pamoja na wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Wataalam wa utafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI).

Akifungua warsha hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaack Mwakisu alisema Serikali inaendelea kuimarisha matumizi endelevu ya ardhi na kuongeza uwezo wa jamii kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia usimamizi bora wa rasilimali za misitu na kilimo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAFORI Dkt. Revocatus Mushumbusi alisema kuwa TAFORI itaendelea kutoa ushauri na utaalamu katika maeneo ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii, kilimo misitu na upandaji miti ili kuhakikisha utekelezaji wenye tija na kufikiwa kwa malengo ya mradi.

Warsha hiyo iliratibiwa na wataalamu wa utafiti wa TAFORI wakiongozwa na Dkt. Numan Amanzi na Dkt. Amani Uisso kwa kushirikiana na waratibu wa mradi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.

Photos from Tanzania Forestry Research Institute's post 22/05/2026

TAFORI Yapokea Pikipiki kwa Ajili ya Kuimarisha Shughuli za Utafiti wa Ufugaji Nyuki Tabora

Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) imepokea pikipiki kwa ajili ya kuimarisha shughuli za utafiti na huduma za ugani katika sekta ya ufugaji nyuki mkoani Tabora.

Pikipiki hizo zimetolewa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani na Siku ya Utundikaji Mizinga Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Kumbukumbu ya Vita mkoani Tabora.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa pikipiki hizo kwa Watumishi na Taasisi za Serikali mkoani Tabora, Mhe. Dkt. Kijaji amesema vifaa hivyo vinalenga kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi, hususani katika kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbali pamoja na kurahisisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali ikiwemo utafiti, usimamizi wa maeneo ya misitu, mapori na shughuli za ufugaji nyuki.

Amesema upatikanaji wa pikipiki hizo utasaidia kuongeza ufanisi katika kuwafikia wafugaji nyuki na wadau wengine kwa haraka zaidi wanapokumbana na changamoto mbalimbali zinazohusiana na sekta hiyo.

Aidha, katika maadhimisho hayo, Mhe. Dkt. Kijaji pia amegawa mizinga 600 kwa vikundi vya wafugaji nyuki ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali kuongeza uzalishaji wa asali mkoani Tabora na nchini kwa ujumla.

Vilevile, Mhe. Dkt. Kijaji amegawa majiko banifu yanayotumia nishati safi kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na kupunguza changamoto ya ukataji holela wa miti katika hifadhi za misitu pamoja na matumizi makubwa ya mkaa.

Maadhimisho hayo yamehitimishwa leo Mei 22, 2026 yakiongozwa na kaulimbiu isemayo: “Uhifadhi wa Nyuki kwa Ustawi wa Mazingira na Taifa Letu.”

Photos from Tanzania Forestry Research Institute's post 22/05/2026

*TAFORI Yapokea Pikipiki kwa Ajili ya Kuimarisha Shughuli za Utafiti wa Ufugaji Nyuki Tabora*

Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) imepokea pikipiki kwa ajili ya kuimarisha shughuli za utafiti na huduma za ugani katika sekta ya ufugaji nyuki mkoani Tabora.

Pikipiki hizo zimetolewa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani na Siku ya Utundikaji Mizinga Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Kumbukumbu ya Vita mkoani Tabora.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa pikipiki hizo kwa Watumishi na Taasisi za Serikali mkoani Tabora, Mhe. Dkt. Kijaji amesema vifaa hivyo vinalenga kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi, hususani katika kuwafikia wananchi waliopo maeneo ya mbali pamoja na kurahisisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali ikiwemo utafiti, usimamizi wa maeneo ya misitu, mapori na shughuli za ufugaji nyuki.

Amesema upatikanaji wa pikipiki hizo utasaidia kuongeza ufanisi katika kuwafikia wafugaji nyuki na wadau wengine kwa haraka zaidi wanapokumbana na changamoto mbalimbali zinazohusiana na sekta hiyo.

Aidha, katika maadhimisho hayo, Mhe. Dkt. Kijaji pia amegawa mizinga 600 kwa vikundi vya wafugaji nyuki ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali kuongeza uzalishaji wa asali mkoani Tabora na nchini kwa ujumla.

Vilevile, Mhe. Dkt. Kijaji amegawa majiko banifu yanayotumia nishati safi kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na kupunguza changamoto ya ukataji holela wa miti katika hifadhi za misitu pamoja na matumizi makubwa ya mkaa.

Maadhimisho hayo yamehitimishwa leo Mei 22, 2026 yakiongozwa na kaulimbiu isemayo: *“Uhifadhi wa Nyuki kwa Ustawi wa Mazingira na Taifa Letu.”*

Photos from Tanzania Forestry Research Institute's post 22/05/2026

MHE. DKT. ABBASI ATEMBELEA BANDA LA TAFORI MAANDALIZI YA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA NYUKI DUNIANI TABORA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hassan Abbasi, leo Mei, 21, 2026 ametembelea banda la TAFORI pamoja na mabanda mengine ya maonesho katika Viwanja vya Kumbukumbu ya Vita mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani na Siku ya Utundikaji Mizinga Kitaifa.

Ziara hiyo imelenga kukagua mabanda ya maonesho na kujionea maandalizi mbalimbali yanayoendelea katika viwanja hivyo ili kuhakikisha utayari wa maadhimisho hayo muhimu yanayolenga kuhamasisha uhifadhi wa nyuki, maendeleo ya sekta ya ufugaji nyuki pamoja na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu.

Kupitia maonesho hayo, TAFORI inaendelea kutoa elimu, huduma za kitaalamu na kusambaza matokeo ya tafiti zinazochangia maendeleo ya sekta ya misitu na ufugaji nyuki nchini.

Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni, “Uhifadhi wa Nyuki kwa Ustawi wa Mazingira na Taifa Letu.”

Want your business to be the top-listed Government Service in Morogoro?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address

Kingolwira
Morogoro

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30